RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

REBECA MALOPE AWAKUBALI GLORIOUS CELEBRATION, UPENDO KILAHIRO NA ROSE MUHANDO KATIKA TAMASHA LA PASAKA-2012. 

AMUOMBEA MAREHEMU STEVEN KANUMBA



Katika tamasha lililofanyika jana katika uwanja wa Taifa wa mpira wa miguu uliopo Mgulani Dar es  Salaam, lilionekana kumpagawisha mwimbaji maarafu wa nyimbo za injili kutoka Afrika Kusini Rebeca Malope. Mwimbaji huyu alipoulizwa na baadhi ya waandishi wa habari kuhusiana na uimbaji uliofanyika steji, naye alisema amependezewa sana na waimbaji wa Glorious Celebration, Rose Muhando na Upendo Kilahiro. 

Glorious Celebration

Rebeca Malope alionekana kupagawa, baada ya Glorious Celebration kuimba wimbo wa Niguse, mikono yake ilionekana juu kama ishara ya kushangilia  pia alijaribu kufuatisha style ya uchezaji wa GC. Baadaye MC alionekana kutaka kukatisha uimbakji wa Glorious Celebration.

Tamasha hili limeandaliwa na Msama Promotoion na lilipambwa na waimbaji mbalimbali kutoka Afrika, baadhi yao ni Anastazia (kiatu), Rose Muhando (nibebe), Upendo Kilahiro, Upendo Nkone, Glorious Celebtration, Solomoni Mukubwa na wengine wengi.

Watu walifurika sana uwanjani na walionyesha uzalendo hasa pale waimbaji walipokuwa wakiingia uwanjani, kelele na vifijo.



Upendo Nkone, Upendo Kilahiro na Christina Shusho wakiingia uwanjani

Katikati muimbaji kutoka Kenya, Emmy Kosgei na Rose Muhando wakiwa uwanjani

Solomon Mukubwa akiwapungia mashabiki

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe akiangalia album ya UTUKUFU KWA MUNGU, Kushoto ni John Merere, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, Solomon Mukubwa, Askofu Gamanywa

Pamoja na umaridadi wa kucheza. Rebeka Malope amehaidi kununua nyumba Tanzania na kuhamia kabisa.

Ephrahim Sekeleti kutoka Zambia

Rose Muhando na Utamu wa Yesu

Tumaini John


Mh. Bernald Membe alipata muda wa kutosha kutoa salamu kwa maaskofu, Raisi na waziri Mkuu, na kuongelea msiba wa Kanumba, akawaomba watu wasimame dakika moja kuomba Mungu amlaze pahali pema peponi na Raisi wa Malawi.

Comments