RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHEMSHA BONGO NA BIBLE


Mtunzi: Rulea Sanga

Maaswali yanatoka katika kitabu cha Marko




Jibu maswali yote kabla hujaangalia majibu yake. Ukiangalia utakuwa umetenda dhmabi kwasababu umekataszwa. Ukishayajibu unaruhusiwa kujisahihisha kwa kuangalia majibu uliyopewa.

MASWALI

  1. (i) Kwanini Petro alisema  “ Rabi, ni vizuri sisi kuwepo hapa; na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, kimoja cha Eliya?

    (ii) Ni sauti gani ilitoka baada ya wingu kutokea na kuwatia vuli Petro Yakobo na Yohana walipokuwa mlimani wakati Yesu akigeuka sura na mavazi yake kung’ara na kuwa meupe mno?

    (iii) Baada ya kusikia hiyo sauti, waliona nini?

  2. (i)Yesu alimwambia nini yule mtu aliyemleta mwanae mwenye pepo bubu ambalo humwaga chini na kusababisha kutoa povu na kusaga meno na kudondoka kutona na wanafunzi wa Yesu kushindwa kumtoa yule pepo?

    (ii)  Yesu alipowaambia wamlete  yule mwenye pepo kuja kwake, pepo lilimfanyeje huyo mwenye pepo?

    (iii)  Yesu alivyomuuliza baba yake na yule mwenye pepo kuwa ni lini alipatwa na pepo, na nini kilikuwa kikimtokea, alijibiwa nini?

    (iv) Baada ya Yesu kujibiwa, huyo mwenye motto mwenye pepo alimuomba Yesu afanye nini juu ya mgonjwa wake?

    (v) Ni maneno gani Yesu alimwambie yule baba wa mototo mwenye pepo lililomfanya bubu, baada ya kuambiwa amhurumie na kumsaidia?

    (vi) Ni kitu gani kilimtokea yule mwenye pepo bubu baada ya Yesu kukemea lile pepo?

    (v) Baada ya pepo kutolewa, Yesu aliwajibu nini wanafunzi wake walipomuuliza, kwanini wao hawakuweza kumtoa huyo pepo bubu?

  3. (i) Yesu alipoulizwa na Mafarisayo kuhusian na mume kumuacha mke wake kwa kumuandikia talaka, je, Yesu alitoa jibu gani?

    (ii) Yesu aliwambia nini wanafunzi wake kuhusiana na wale wanawaacha wake zao na kuoa wengine?

  4. (i) Baada ya wanafunzi kutaza watoto wadogo kumgusa Yesu, Yesu aliwaambia nini hao wanafunzi kuhusiana na watoto wadogo?

    (ii) Yesu aliwaonya nini hao wanafunzi kuhusiana na kuwakataza watoto wadogo wasimguse?

    (iii) Yesu alifanya nini kwa hao watoto wadogo baada ya kuwaonya wanafunzi wake waliokuwa wanawakatza watoto hao wasimguse Yesu?

  5. (i) Yesu alijibu nini yule mtu aliyemkimbilia na kupiga magoti mbele zake hasa pale aliposema “Mwalimu Mwema” wakati akitaka kujua ni jinsi gani afanye kurithi ufalme wa Mungu?

    (ii) Ni kitu gani Yesu alimwambia afanye  yule mtu aliyepiga magoti mbele za Yesu ili aweze kurithi ufalme wa Mungu hata kama hajawahi  hakuzini, hakuua, hakuiba, hakuhusudia uongo, hakudanganya, aliwaheshimu baba na mama yake tangia utoto wake?

MAJIBU

  1. (ii) Kwasababu walikuwa na hofu na hawakujua la kunena kutoka na vile kutokana na Yesu kugeuka sura mbele yao, mavazi yake yakamete-meta na kuwa meupe mno jinsi asivyoweza dobi duniani kuyafanya meupe. Haya yalitokea pale mlimani ambapo Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana faraghani. (Marko 9:2-6)

    (ii) “Huyu ni mwanangu mpendwa msikilizeni yeye” (Marko 9:7)

    (iii) walimwona Yesu pekee yake. (Marko 9:8)

  2. (i)Yesu aliwajibu, akasema, “Enyi kizazi kisichoaamini, nikae nanyi hata lini, nichukuliane nanyi hata lini?”  (Marko 9:19)

    (ii)  Yule pepo alimtia kifafa, naye akaanguka chini, akagaagaa, akitokwa na povu. (Marko 9:20)

    (iii) Yesu alijibiwa kuwa alipatwa tangia alivyokuwa motto, na mara nyingi ametupwa katika moto, katika maji, amwangamize. (Marko 9:21)

    (iv) Alimwomba Yesu aseme neon lolote na amhurumie na kumsaidia. (Marko 9:22)

    (v) Yesu alimwambia akisema, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. (Marko 9:23)

    (vi) Huyo mwenye pepo akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka na yeye akawa kama amekufa (Marko 9:26)

    (v) Yesu akawaambia “ Namna hii hiwezi kutoka kwa neon lolote, isipokuwa kwa kuomba. (Marko 9:29)

  3. (i) Yesu aliwambia, Kwasababu ya ugumu wa mioyo yenu, Musa aliwandikia amri hii. Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mke na mume. Kwasababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye  ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja, hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe. (Marko 10:8-9)

    (ii) Yesu aliwaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na na kuoa mwingine azini juu yake, na mke akimwacha mumewe na kuolewa na mwingine , azini. (Marko 10:11)

  4. (i)  Yesu alichukizwa sana, na alimwaambia wanafunzi wake, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie kwa maana, watoto kama hawa ufalme wa Mugu ni wao. (Marko 10:14)

    (ii) Yesu akawambia, Amini na wambieni, Yeyote asiyekubali ufalme wa Mungu kama motto mdogo hatauingia kabisa. (Marko 10:15)

    (iii) Yesu akawabariki hao watoto. (Marko 10:16)

  5. (i) Yesu akasema, kwanini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja ndiye Mungu. (Marko 10:18)

    (ii) Yesu alimwambia, “Enenda ukauze ulivyonavyo vyote, uape maskini nawe utakuwa na hazina mbinguni, kasha njoo unifuate. (Marko 10:21)





Comments