MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MCHUNGAJI GETRUDE RWAKATRE ANAKUALIKA KATIKA NYUMBA YA MUNGU MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASSEMBLIES OF GOD

Mwandishi: Rulea Sanga

Jumapili hii ni siku ya mlipuko wa moto katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B kwa Mch. Dk. Getrude Rwakatre.
Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblies of God, Getrude Pangalile Rwakatare

Unakaribishwa kuja kupokea baraka zako na kumuangamiza shetani anayekusumbua katika maisha yako. Kufika kwako ndiko kutafanya ibada kuwa nzuri na  Mungu kuifurahia ibada hiyo. Kukosa kwako kutafanya kanisa kuwa tupu na shetani atajiinua na kuonekana yeye anaweza kumshinda Mungu.

Njoo na rafiki yako na ndugu yako. Ibada itaanza saa 3 asubuhi na kuendelea. Umefika wakati wa kuwa mashabiki wa Yesu na kupenda kila kitu ambacho Mungu anataka sisi kama watoto wake tufanye.

Katika ibada hii kutakuwa na waimbaji kama Bahati Bukuku atakaeimba nyimbo tatu, Happy Kwaya na Joys Bringers za Kanisa la Mlima wa Moto. Mungu tunaamini siku ya Jumapili ataonekana LIVE kwa jina la Yesu.

Mchungaji kutoka Kenya Junior Francis atakuwepo katika ibada ya hii akiwa na mchungaji mwenyeji Dr. Getrude Rwakatre. "Tumejipanga vizuri katika kazi ya Mungu", walisema

Mbali na ibada kutakuwa na semina ya siku tano ambayo itaanza Jumapili hii mpaka mwisho wa wiki.

"Nakuomba ufike, tusimudondoshe Yesu jamani."

Mungu akuwezeshe upate nauli, afya, msukukumo wa kufika kanisani. Kanisa letu liko Mikocheni B, panda gari lako au kama unatumia daladala shuka Mwenge na ukifika kwenye mtaa angalia barabara inayoelekea kiwanda cha Coca Cola na utakuta bajaji nyingi zinaelekea huko. Pia kuna magari ya St. Marys yatakupakia bure mpaka kanisani

MUNGU WETU AKUBARIKI
0