RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NDOTO YANGU (RULEA SANGA) KUHUSU KUMPONYA MTU MWENYE MAPEPO


Mwandishi: Rulea Sanga
UKISOMA NDOTO YANGU INAWEZA KUKUJENGA KIIMANI

Jana nimeota ndoto ambayo iliniinua kiimani na kihuduma. Ningependa tushirikiane kwa kujua makusudi ya Mungu kwa watoto wake.



Nikiwa kitandani, usiku wa jana nimeota ndoto, na hivi ndivyo nilivyoota :

Nilikuwa nimechelewa kuingia katika ibada kanisani na kukuta waumini wenzangu wamjaa kanisani. Ibada ilikuwa inaendelea na mimi nikisikiliza Neno la Mungu. Ibada ilipoisha watu walitoka kanisani na kuelekea majumbani kwao, lakini kulikuwa na akina dada wanne wamebaki kanisani wakiwa wamekaa katika viti vya mbele kabisa. Kati ya hao wadada wanne akaja dada mmoja mzuri sana akiwa amevalia vazi la kiislamu la rangi nyeusi akaomba nimuombee, nilimkubalia yule dada kumuombea. Nilipoaanza maombi yangu, nikatamka jina la Yesu, yule dada alianguka chini na kuanza kupiga kelele, huku sura yake ikionyesha kudharau kile ninachoomba. Nikaendelea na maombezi huku nikitamka maneno ambayo “Wise men” wa Nabii T.B. Joshua hutumia ya “Out Out Out in the name of Jesus”

Nikiwa katika maombezi na kukemea nikamuona mchungaji wa Mlima wa Moto akiniangalia na kupenda huduma yangu niliyokuwa naifanya kwa yule dada mwenye mapepo. Niliendelea kukemea kwa muda mrefu sana bila mafanikio. Wale rafiki zake ambao walikuwa pamoja na huyu dada walikuwa wananiangalia nikikemea mapepo. Baadae hawa akina dada waliamuma kutoka na kwenda nje kumsubiria rafiki yao; walisimama katika gari jeupe wakipiga story. Akina dada hao walikuwa wamevalia mavasi ya kiislamu na kila mmoja alikuwa amvaa vazi la rangi yake (sky blue, nyeusi na Orange ya kupauka).

Niliendelea na maombezi kwa muda mrefu sana mpaka nikahisi kuchoka huku jasho likinitoka. Mikono ya shati langu niliikunja kutoka na jasho ambalo nilikuwa napata. Pepo likawa linakataa kutoka na wakti huohuo dada huyo alikuwa ni mtu asiyetulia, anatembea tembea huku na kule-hashikiki.

Baada ya muda Fulani, yule dada alidondoka maeneo ya madhabahuni karibu na dirisha. Nikachungulia nje nikaona wale wadada wanaendelea na story zao pale kwenye gari nyeupe. Yule dada mwenye mapepo pale alipodondoka alilala usingizi mzito sana na nikahisi labda amezimia, kwa maana alitulia sana bila ya kujitingisha wala kuhema kwa vujo kutoka na “movement” alizokuwa akizifanya wakati anaombewa. Niliogopa sana. Nguo za huyo dada zilikuwa za rangi ya orange iliyopauka na ni nzuri sana. Nikatazama nje kwa kuitia lile dirisha, nikaona wale rafiki zake wakishauriana kuondoka. Nikarudi tena kwa yule dada na kumuomba Mungu amfungue na aweze kuongea, na mkono wangu nikawa nauzungusha katika kichwa chake. Nikamwita rafiki yake mmoja ili aone kazi ya Mungu inavyofanya kazi ya uponyaji, na yule dada alipofika alishangazwa sana na akawa na uwoga akidhani labda amekufa.

Baada ya muda kidogo, yule dada akaamuka usingizini akiwa hajielewi aliko. Nikamuuliza maswali ili kujua kama ufahamu wake umekuja. Yule dada alinijibu sawasawa na nilivyokuwa namuuliza, na hapo niligundua kuwa amefunguliwa. Nikamshukuru Mungu kwa uponyaji. Dada aliyekuwa anaombewa akaniuliza kwani hapo alipo yuko  wapi? Nikamjibu “Uko kanisani”, akaangalia juu na kuniambia kanisa lenu ni zuri linapendeza, hongereni kwa maendeleo yenu. Kanisa lilionekana lina rangi ya orange. Kumbuka huyo dada aliyombewa hilo ni kanisa lake la kila siku na sio mara yake kuingia, nab ado anashangaa lilivyo zuri. Kutokana na kushangazwa kwa kwa huyo dada kuhusu kanisa, nikagundua kuwa dada huyo alifungwa ufahamu wa kujua mazuri ya Mungu na kazi ya Mungu kutoka na shetani kumfunga.

Nilipomaliza zoezi la huyo dada mwenye mapepo, rafiki yake niliyemwita aje kumuangalia rafiki yake, aliomba nimuombee. Nikwamwambia akae katika gazi za madhabahuni pale alipokuwa amelala mwenzie baada ya kuanguka. Nikanyoosha mikono yangu na kumgusa katika kichwa chake, nilipotamka YESU yule dada akalalamika sana akiomba nimwache huku akikataa mikono yangu isoiguse kichwa chake wala kuelekeza kwake. Dada alionekana kupagawa na nguvu za giza. Nilipogundua hivyo nikamuomba Mungu atulize yale mapepo ili nimwambie yule dada aje kesho kwa maombi. Mapepo yalitulia na nikamwambia tuonane kesho. Na hii ilitokana na uchovu wa yule dada wa kwanza.

Ndoto yangu iliishia hapo.

Comments