RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMA AFRICA INAKUSHUKURU Mwl. MWAKASEGE KWA UJIO WAKO KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI DAR na UWANJA WA RELI ARUSHA

Mwandishi: Rulea Sanga

Ruma Africa na uongozi mzima inakushukuru sana Mwalimu Mwakasege kwa kazi ya Mungu unayofanya kuokoa roho za watu zilizokufa kujua Neno la Mungu. Kazi yako itaenda kuwainua watu wengi katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam na viwanja vya Reli Arusha. Kazi yako itapimwa na Mungu na utaona matunda yako mtumishi wa Mungu. Nasi wasikilizaji tutapimwa na kuona vile ulivyotufundisha kama tulivifanyia kazi.

Ndugu yangu nakuomba kama blogger wako, Rulea Sanga kupenda kufanya kazi ya Mungu kwa namna yoyote ile. Kuna nmambo mengi unaweza kufanya kwa kazi ya Mungu. Mwakasege hawezi kutengeneza blogu kama mimi na kusambaza neno la Mungu kwa kupitia blogu, lakini Mungu amempa karama ya kuwa mwenye hekima na maneno yenye kugusa maisha ya watu.

Watanzania tumezoe kumuona mtumishi wa Mungu katika viwanja vya Biafra Dar es Salaam, lakini kipindi hiki hatakuwepo mahali pale na badala yake atafanya huduma katika viwanja vya Jagwani dar es Salaam.

Nakuhimiza mdau wangu, fika mahali pale ili uweze kupokea baraka zako. Hatujui kwanini Mungu ameamua kumpeleka mtumishi katika viwanja vya Jangwani na sio Biafra. Kuna chakula kipya na kitamu ambacho ameamua watoto wake tukale katika viwanja vya jangwani. Wewe kama unanjaa na unaona kuna rafiki yako ananjaa na anatamani kula chakula mualike.

Kutakuwa na kipindi cha vijana wa chuo,sekondari na walioko nyumbani siku ya jumamosi tarahe 15/9/2012 kwa Arusha(uwanja wa reli) na 29/9/2012 kwa Dar es salaam(uwanja wa jangwani) kwanzia saa tatu asubuhi mpaka saa sita mchana. Mungu awabariki sana na tunashukuru kwa maombi yenu na tunaendelea kuwaombea.

Comments