RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA KKKT LATANGAZA SIKU YA MAOMBI NCHINI TANZANIA-28 OCTOBA 2012


Kufuatia matukio ya Uvunjifu wa Amani unaofanywa na kikundi cha watu wachache kwa mwamvuli wa "dini". Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limetoa Waraka Elekezi Wa Wachungaji Wake Wote Tanzania kuelekeza kuwa siku ya tarehe 28 October, 2012 ni siku ya Kufunga na Kuomba kwa ajili ya Amani nchini Tanzania.

Kanisa la KKKT linakuwa kanisa la Kwanza Tanzania kupitisha siku ya Kikanisa la Kufunga na Kuomba kwa ajili ya Amani Ya Nchi ilivyo Sasa.

Blog hii ambayo imefanikiwa kuutia machoni waraka huo uliotumwa na Maaskofu Dayosisi zote KKKT Wakuu wa Vituo vya Kazi za Umoja, KKKT na nakala yake kutumwa Manaibu Katibu MkuuK,Wasaidizi wa Ma aaskofu, DayosisizoteK,K KT, Makatibu Wakuu Dayosisizote kuwaelekeza kwamba tarehe 28 Octoba ni Siku ya Kufunga na Kuomba. Waraka huo umeelekeza "Kufuatia matukio ya kuchoma Makanisa yaliyotokea hivi karibuni,barua  inawataarifu kuwa siku ya Jumapili tarehe28 Oktoba 2012 imepangwa kuwa siku maalum ya kuornbea amani katika nchi yetu.Pamoja na mambo mengine yaliyokwishakupangwa kufanyika siku hiyo ( 28 Oktoba2012)' tafadhali siharika, mitaa na Vituo vya Kazi za Umoja vyote vya Kanisa letu vifanye maombi  hayo"

Kwa Mujibu wa Barua hiyo Ya Mtendani Mkuu wa Kanisa la KKKT inawataka Waumini wa Kanisa hilo kuendelea Kuhimizwa Kufunga na Kuomba Kwa Kadri Roho Wa Bwana atakavyowaongoza kuombea amani ya Tanzania. Blog ikunukuu sehemu ya mwisho ya barua hiyo inaeleza kuwa "Baada ya maombi ya siku hiyo,Washarika wahimizwe kuendelea kufunga na kuomba kadiri Roho wa Mungu atakavyowaongoza" mwisho wa kunukuu.

Ipo haja na Kanisa la Tanzania Kuungana Sambamba na Kanisa la Kiinjili La Kilutheri Tanzania katika Kuombea amani ya Tanzania.

Comments