RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MKANDAMIZAJI NA ORIGINAL COMEDY NDANI YA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID ARUSHA KESHO


Masanja Mkandamizaji alipokuwa akihubiri mkutano jijini Mbeya hivi karibuni.                 
Mwigizaji maarufu nchini ambaye ameyakabidhi maisha yake kwa Yesu, Emanuel Mgaya jina la kazi Masanja Mkandamizaji au waweza kumwita Mchungaji mtarajiwa, hapo kesho anatarajia kuzindua album yake ya ''HAKUNA JPYA'' DVD kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha akisindikizwa na waimbaji mbalimbali pamoja na waigizaji wenzake kutoka kundi la maarufu la vichekesho nchini la Original Comedy.

Kati ya waimbaji watakaokuwepo katika uzinduzi huo ni pamoja na Annastazia Mkabwa a.k.a Kiatu kivue, Faraja Ntaboba, Christina Mbilinyi, Bubujiko Choir kutoka kaloleni pamoja na kwaya nyinginezo, huku tamasha likitarajiwa kuanza majira ya saa 6 na kumalizika saa 12 jioni kiingilio wakubwa 4,000 na watoto 2,000. Hii itakuwa mara ya pili kwa mwimbaji na mwigizaji huyo kuzindua DVD yake, kwani alishafanya hivyo huko mkoani Iringa mapema mwaka huu. Pia kwasasa ameanza kuandaa mikutano yake yenye lengo la kuwaleta watu kwa Mungu muhubiri akiwa niyeye mwenyewe na tayari amefanya mikutano miwili mwezi uliopita mikoa ya Mbeya na Iringa.

                 

Comments