RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWILI WA MAREHEMU SHARO MILIONEA ULIVYOHARIBIKA

Rumafrica inawapa pole wafiwa wote wa marehem Sharo Milionea ambaye aligusa watu wengi kwa kipaji chake cha uchekeshaji. Pia tunawapa pole waumini wote wa Kiislamu kwa kumpoteza mmoja wa waumini wake.

 Mwili wa marehemu Sharo Milionea umeharibika vibaya kama unavyoonekana pichani hapao juu pichani ni wazi ilikuwa ajali mbaya.

Hili ndilo gari aina ya Toyota Harrier lenye namba T278 BVR ilipinduka na kusababisha ajali iliyopelekea kifo cha msanii Sharo milionea USIKU WA JANA MIDA YA SAA MBILI USIKU

Hapo jana usiku mtandao wa jamii wa Facebook kwa upande wa watumiaji nchini Tanzania uligubikwa na taarifa za masikitiko juu ya kifo cha mwigizaji ambaye amejizoelea mashabiki lukuki kupitia matangazo ya runinga ya mtandao wa Airtel aitwaye Hussein Mkiety a.k.a Sharo Millionea ambaye matangazo yake amekwenda sambamba na mwigizaji mwingine nguli King Majuto.

Kutokana na taarifa za kifo cha msanii huyo aliyefariki kwa ajali ya gari alilokuwa akiliendesha mwenyewe akittokea jijini Dar es salaam kwenda Tanga na kuacha njia kisha kupinduka kutokana na hali ya hewa ya mvua na gari kuwa mwendo kasi, haya ni baadhi ya yale yaliyoandikwa na watumiaji hao ambao wengi wao wanamwamini Mungu.

MATANGAZO YALIYOMUINUA SHARO

Comments