Select Menu

News

USIKOSE IJUMAA HII MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

USIKOSE IJUMAA HII MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

MLIMA WA MOTO JUMAPILI HII

MLIMA WA MOTO JUMAPILI HII

SARAH KUZINDUA ALBAM YAKE JUMAPILI HII

SARAH KUZINDUA ALBAM YAKE JUMAPILI HII

MCH. BURTON SANGA

MCH. BURTON SANGA

TTCL

TTCL

GEPF

GEPF

VIGAE TANGAZO

VIGAE TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

AZAM TV

AZAM TV

RUMAFRICA NA HABARI ZA GOSPEL: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA Online MAGAZINE: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

Rumafrica. Powered by Blogger.

RUMAFRICA Online TV: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA: MATANGAZO: Bonyeza alama nyekundu

ELIMIKA NA RUMAFRICA

RUMAFRICA MTAANI

MLIMA WA MOTO ONLINE TV NA HABARI MBALIMBALI ZA MLIMA WA MOTO

RUMAFRICA VIDEO

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UENDESHWAJI WA UDAHILI - ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA

(TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES – TCU)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UENDESHWAJI WA UDAHILI - ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013

UTANGULIZI

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (‘Tanzania Commission for Universities’-TCU) ikishirikiana na Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi (‘National Council for Technical Education’ - NACTE) pamoja na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi Elimu ya Juu (Higher Education Students Loans Board) inapenda kuutarifu umma kuhusu utaratibu wa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2012/2013 kupitia mifumo ya “Pre-entry”, “Mature Age Entry”, “Equivalent Qualifications” na mfumo wa pamoja wa udahili (‘Central Admission System’) na utaratibu wa mikopo kama ifuatavyo:

MFUMO WA UDAHILI KUANZIA MWAKA 2012/13
1.1 Utaratibu wa Kuendesha Program za “Pre-entry” na “Mature Age Entry”

Kuanzia mwaka huu 2012, vyuo vyote vitakavyotaka kuendesha mafunzo ya awali kabla ya mwombaji kustahili kudahiliwa ili kuweza kujiunga na programu za elimu ya juu (pre-entry programmes) pamoja na kuendesha mitihani ya kupitia mfumo wa “Mature Age Entry” vinatakiwa kuwasilisha programu hizo Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa uhakiki na kupata kibali. Programu hizo ni lazima ziendeshwe kwa muda wa mwaka mmoja. Hali kadhalika kwa upande wa mitihani kupitia mfumo wa mature entry, Tume kwa ushirikiano na Baraza, kwa pamoja wataandaa na kuratibu utaratibu wa mitihani katika vituo maalum kikanda ili vyeti vitakavyotolewa viwe na ulinganifu unaostahili na hatimaye kuweza kutumika katika udahili wa sifa linganishi katika vyuo mbalimbali.

Vyuo vinatakiwa kuandaa programu za mifumo ya “Pre-entry” na “Mature Age Entry” na kuziwasilisha Tume na Baraza ili zihakikiwe kwani mwaka wa masomo kwa kusudi hili utaanza mwezi Agosti 2012/2013. Kwa utaratibu huu, watakaofanya mafunzo hayo watatakiwa kufanya mitihani yao na kujiunga na masomo ya elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2013/2014.


Kwa taarifa hii, mwaka 2012/13 hakutakuwapo na udahili wa wanafunzi kwa mfumo wa “Pre-Entry” na “Mature Age Entry”.


1.2 Utaratibu wa Udahili Kupitia Mfumo wa Pamoja (Central Admission System)


Waombaji watakaopitia mfumo wa pamoja wa udahili (CAS) wamegawanyika katika makundi manne, ambapo waombaji wa kundi (i), (ii) na (iii) watatambuliwa kama “Direct Applicants” na kundi (iv) watatambuliwa kama “Indirect Applicants”

Waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita katika kipindi cha miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka huu.
Waliohitimu mafunzo ya diploma ya elimu ya ufundi (NTA level 6) kutoka vyuo vinavyotambulika na NACTE miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka huu;
Waliohitimu mafunzo ya Diploma ya Ualimu (kutoka vyuo vinavyotambulika) katika kipindi cha miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka huu.
Waombaji ambao sio wa moja kwa moja (Indirect Applicants) ni wote waliohitimu kidato cha sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi (NTA level 6) na Diploma ya Ualimu katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili iliyopita (kuanzia 2009 kurudi nyuma).

1.2 Waombaji Watakaowasilisha Maombi yao Moja kwa Moja Vyuoni
Waombaji watakaowasilisha maombi kupitia vyuo husika ni wenye sifa linganishi (Equivalent Qualifications) yaani wenye vyeti vya Astashahada na Diploma ambazo hazitambuliwi moja kwa moja na NACTE. Ili kukamilisha udahili, wanashauriwa kuwasiliana na NACTE ili vyeti vyao vitambuliwe na kusajiliwa kabla udahili haujaanza.

Vyuo vinavyofundisha programu mbalimbali katika ngazi ya Astashahada na Diploma ambavyo havina usajili wa NACTE/NECTA vinatakiwa kuwasilisha matokeo ya wanafunzi wao NACTE haraka iwezekanavyo ili matokeo hayo yaweze kutumika katika utambuzi wa vyeti vya wanafunzi husika.

MUDA WA UDAHILI KWA MAKUNDI MBALIMBALI
Muda wa maombi wa kuwasilisha maombi ya udahili kwenye CAS umegawanyika katika makundi matatu kama ifuatavyo:

Kundi la Kwanza – (1 Aprili mpaka 30 Aprili 2012)
Waombaji wote waliomaliza kidato cha sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi (NTA level 6), na Diploma ya Ualimu kuanzia mwaka 2011 kurudi nyuma wataanza kuomba udahili kuanzia Aprili 1, 2012 hadi 30 Aprili 2012.Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

AIRTEL YAFANYA SEMINA KWA MASHIRIKA NA SEKTA MBALIMBALI NCHINI KUHUSU AIRTEL MONEY
Mkurungezi wa fedha wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Kalpesh Mehta akitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa mashirika na wadau mbalimbali walioalikwa na kuhudhuria seminar hiyo iliyofanyika leo na kuendeshwa kwa siku mbili katika makao makuu ya Airtel , lengo likiwa ni kuwaeleimisha wafanyabiashara na mashirika mbalimbali jinsi huduma ya Airtel money inavyoweza kutoa suluhisho la matatizo yanayowapata katika kuendesha biashara zao.
Mkurungenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam Elangallor (Kushoto) akiongesha kwa vitendo jinsi gani huduma ya Airtel money inavyofanya kazi na kutoa shuluhisho kwa changamoto wanazozipata katika kuendesha biashara kwa wawakilishi kutoka katika makapuni mbalimbali waliohudhuria semina hiyo iliyofanyika Makao makuu ya Airtel, pichani anayefata ni Mkurungezi wa fedha Kalpesh Mehta na Meneja huduma Airtel money Asumpya Naligingwa.
Mkurungenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam Elangallor akitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa wawakilishi kutoka katika makampuni mbalimbali waliohudhuria semina hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel nakuhudhuria na wadau mbalimbali na waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa mahusiano wa Airtel Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa semina ya Airtel money inayotolewa kwa makapuni mbalimbali leo kwa muda wa siku mbili, uzinduzi huo ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na wadau wengi na waandishi wa habari
Wadau waliohudhuria wakichangia hoja Mmoja wa wakilishi kutoka katika makampuni yaliyohudhuria semina ya huduma za Airtel money akichangia hoja wakati wa semina hiyo iliyozinduliwa rasmi leo na kuendesha na Mkurugenzi wa Airtel Sam Ellangallor na Mkurugenzi wa fedha Kalpesh Meltha katika ofisi za makao makuu ya Airtel.


Mkurungenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam Elangallor (kushoto) na Mkurungezi wa fedha Kalpesh Mehta kwa pamoja wakitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa wawakilishi wa makampuni mbalimbali yaliyoalikwa kupata mafunzo juu ya faida na matumizi ya huduma hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali za uendeshaji wa biashara zao. Semina hiyo semina hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel nakuhudhuria na wadau mbalimbali na waandishi wa habari.

-----------------------------
Katika kuhakikisha huduma ya pesa mkononi inawafikia watanzania wengi Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Leo imeendesha semina ya huduma ya Airtel money kwa wadau na sekta mbalimbali wakiwemo wadau wa usafirishaji, asasi za kifedha, wakuu wa shule na vyuo vya elimu ya juu kwa lengo la kupambanua faida za kutumia huduma mpya ya Airtel Money katika shughuli zao zinazohusiana na maswala ya kulipa au kupokea fedha.

Akizungumza wakati wa semina iliyohudhuriwa na wadau hao na kufanyika katika makao makuu ya Airtel Tanzania Afisa Mkuu wa Biashara Walingo Chiruyi alisema “lengo la semina hii ni kutaka kujadiliana na wadau wetu faida za kuitumia huduma yetu hii mpya ya Airtel Money katika shughuli zao za kila siku.

Tumegundua huduma hii ni nyenzo muhimu sana katika kuweka urahisi usalama zaidi pamoja na kupunguza hatari zinazotokana na kutembea na fedha nyingi au kukaa ofisini na fedha nyingi kwa lengo la kuzitumia katika shughuli za wiki nzima au kulipa mahitaji mbalimbali.

Airtel Money ni suluhisho la kufanya hayo yote na ndio maana leo hii tumekaa pamoja kwa lengo la kuweka kila kitu bayana kwa wadau hawa muhimu kwetu! Aliendelea kusema Bw,

Akitoa maelezo zaidi ya jinsi ya kutumia huduma ya Airtel money ambapo kwa kupitia huduma hiyo wateja wanaweza kulipa Ankra kama vile Ada ya shule, Mishahara ya wafanyakazi au vibarua, Kufanya makusanyo ya mauzo ya siku, kulipia huduma za DSTV, Luku, bili ya Dawasco, kulipia visa ya USA, pamoja na kutuma na kupokea hela ndani na nje ya nchi.

Aidha kwa wafanya biashara za usafirishaji huduma ya Airtel money itawasaidia katika kupunguza risk za wizi wa fedha na kuwaakikishia usalama madereva wakiwa safarini kwani malipo yote ya bidhaa baada ya usambazaji hayatafanyika tena kwa pesa taslimu bali kwa kupitia huduma ya Airtel money.

Kwa mabasi ya abiria wateja sasa wataweza kufanya booking na kulipa nauli kwa kupitia huduma ya Airtel money ambapo mteja hatakuwa na ulazima wa kutembelea kituo cha basi kukata tiketi na kulipia gharama za nauli.

Huduma ya Airtel money pia itapunguza gharama zilizopo katika kupata huduma za kifedha, na kwakupitia mtandao wetu ulioenea zaidi nchi nzima na mawaka waliosambaa kote tuna uhakika wa kuwafikia watanzania wengi zaidi walioko mjini na vijijini aliongeza Bi, Kazimoto.

Airtel hivi karibuni ilizindua na kuboresha huduma ya Airtel Money pesa mkononi na mpaka sasa watanzania wengi wamefaidi kwani imeweza kutoa ajira kwa watanzania wengi kwa kupitia uwakala hivyo wananchi wengi wameweza kujipatia mapato kwa kupitia huduma hii, Huduma ya Airtel money sasa ina mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa nchi nzima hivyo ili kukamilsha upatikanaji wa huduma hii ya kisasa na rahisi zaidi.

Posted by CATHBERT ANGELO
POSHO ZA WABUNGE HAZIJAPANDA- RAIS JAKAYA KIKWETE ATOA UFAFANUZI
Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge: Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku. 


Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka kutoa ufafanuzi ufuatao: 


Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi. 


Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:


Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili. 


Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.


Imetolewa na:


Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Januari, 2012
MTUME NA NABII MWINGIRA ATIWA MBARONI DAR
KIONGOZI wa Kanisa la Efatha, Nabii na Mtume Josephat Mwingira amekamatwa na polisi katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam, akituhumiwa kuharibu mali za mfanyabiashara, Zain Sharifu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, ACP Charles Kenyela, Mwingira alikamatwa wiki iliyopita na kushikiliwa kituoni hapo.
Hata hivyo, Kenyela alisema, Mwingira alidhamiwa baada ya kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za kuvunja na kuharibu mali ndani ya Kiwanda cha Uchapaji cha Afroplus kinachomilikiwa na mlalamikaji.

“Tumemkamata kiongozi huyo ili atoe ufafanuzi wa kina baada ya kupokea malalamiko hayo, “ alisema Kenyela alipozungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita ofisini kwake.
Kenyela alisema, mashtaka hayo yalifikishwa polisi na Zain, Januari 8, mwaka huu, akidai kwamba walinzi binafsi wa kiongozi huyo wa kanisa, walivamia kiwandani kwake na kuharibu mali baada ya kufanya fujo.

Aliongeza kuwa polisi baada ya kupata taarifa hizo, walikwenda eneo la tukio kushuhudia na kukuta mali zilizoharibiwa, hivyo walimtaka Mwingira kufika polisi ili atoe ufafanuzi lakini alikaidi ndipo polisi ikatumia nguvu kumkamata.

“Alipoulizwa Mwingira kuhusu madai hayo alijitetea uwa eneo hilo ni mali halali ya Efatha tangu Juni 17, 2005, baada ya kulinunua kutoka kwa mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Mangula, hivyo anasubiri tamko la Mahakama ya Ardhi Tanzania ambako shitaka limepelekwa,” alisema.
Baada ya Mwingira kuhojiwa kituoni hapo, Kenyela aliwakutanisha na Zain ambaye ni mlalamikaji na kuwataka wasiendelee kugombana, badala yake wasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu kesi hiyo. 
Kamanda Kenyela alifafanua kuwa mwanamke aliyemshitaki Mwingira ni mmoja wa wamiliki 11 wa viwanda vilivyokuwa ndani ya Kitalu namba 90, Mwenge, Dar es Salaam.

Awali, Mwingira alisema, aliwataka wamiliki wa viwanda hivyo kuhama ili kupisha upanuzi wa kanisa na viwanda 10 vilitekeleza ombo hilo.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa makampuni 10 ambayo yalitakiwa kuhama na Mwingira na kutekeleza ni Metal Works, Timber Malt Tech, Auto Ran Makongo, Container Global, Simon Engineering, Safe Man, Profession Investigation, Elbe Ltd, Zana za Kilimo Mbeya na Kilimanjaro Machine Tools Ltd.

Januari 17 mwaka huu, katika toleo lake namba 721 gazeti hili liliripoti kusakwa kwa Mwingira na askari 20 waliofika kanisani kwake kwa lengo la kumkamata.
Askari hao waliokuwa katika magari mawili aina ya Land Rover ‘Difenda’ walifika kanisani kwa Mwingira baada ya kupata taarifa za kutokea kwa fujo kati ya wafuasi wa kanisa na wafanyakazi wa viwanda cha Afroplus kinachopakana na kanisa hilo, Mwenge, Dar lakini walimkosa.

Kamanda Kenyela alisema alimtuma mkuu wa polisi wa wilaya (OCD) kumpelekea Mwingira barua ya wito ili afike ofisini kwake na kutoa onyo kwamba kama akikaidi, wao polisi wasilaumiwe.
Baadhi ya wananchi waliokuwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay baada ya kumuona Mwingira walisema ni kitendo cha aibu kwa viongozi wa makanisa ya kiroho kufikishwa polisi.

“Siyo Mwingira tu, tumekuwa tukiona viongozi wengi wa makanisa ya kiroho wakifikishana polisi na watu au wao kwa wao, ningeshauri haya mambo wayamalize kwa kuelewana uraiani. Wana uwezo wa kuombea matatizo, hilo linawashinda nini? Zamani ilikuwa ni mwiko kuona kiongozi wa dini akifika polisi kulalamika au kulalamikiwa,” alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Frida Gabriel aliyedai kuwa ni mlokole.

DARASA ELIMU YA UKIMWI KWA WANAHABARI LAENDELEA UKUMBI WA MADAKTARI MBEYA -LIVE


waratibu wa TACAIDS kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini
Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Ruvuma akieleza hali halisi ya UKIMWI mkoani kwake
Wawezeshaji wa TACAIDS Taifa wakifuatilia mrejesho wa UKIMWI kutoka kwa waratibu wa TACAIDS
Darasa linaendelea kwa wanahabari kunolewa
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya utangazaji mikoa ya Iringa,Mbeya,Rukwa na Ruvuma wakiwa darasani

Wawezeshaji wa kitaifa wakiwa katika harakati za semina
wanahabari wakiwa katika semina


DARASA ELIMU YA UKIMWI KWA WANAHABARI LAENDELEA UKUMBI WA MADAKTARI MBEYA -LIVE


waratibu wa TACAIDS kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini
Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Ruvuma akieleza hali halisi ya UKIMWI mkoani kwake
Wawezeshaji wa TACAIDS Taifa wakifuatilia mrejesho wa UKIMWI kutoka kwa waratibu wa TACAIDS
Darasa linaendelea kwa wanahabari kunolewa
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya utangazaji mikoa ya Iringa,Mbeya,Rukwa na Ruvuma wakiwa darasani

Wawezeshaji wa kitaifa wakiwa katika harakati za semina
wanahabari wakiwa katika semina

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS