RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

AMPATA MWANAE BAADA YA MIAKA 50 TANGU APOKONYWE AKIWA NA WIKI SITA



Teresa na mwanae David, picha kwahisani ya Good newspaper.

Mwaka 1958 nilijifungua mtoto wa kiume nilimpenda sana lakini nilikuwa sijaolewa pia nikiwa na umri chini ya miaka 21 hali ambayo inamaanisha nilikuwa chini ya mamlaka ya wazazi wangu, ambao walinifanya nigawe mtoto wangu na kuchukuliwa na watu wengine. Mara ya mwisho kumuona mwanangu ilikuwa wakati anawiki sita tangu nijifungue na kulazimika kumgawa kwa watu wengine, kitendo hicho ndicho kilinisukuma mimi kuanza maombi ili Mungu anisaidie niweze kumuona mwanangu kwa mara nyingine najua maombi sio siku zote unaweza kupata majibu kwa muda mfupi au wiki moja baada au hata baada ya mwaka, maombi yangu yamejibiwa baada ya miaka 51, Mungu alikuwa akitenda kazi" Anaeleza Teresa Pullman's mwanamama ambaye anasema alizaliwa katika familia isiyo ya Kikristo lakini aliweza kuhudhuria shule ya jumapili(Sunday school), alisoma katika shule ya Kikristo ambako alifundishwa kuomba lakini aliachana na maombi baada ya kumaliza shule, na alipopata ujauzito alipelekwa kuishi katika nyumba ya Kikristo kwa akinamama wasioolewa ambako walipata faraja na kuhudhuria kanisani nakumfanya afikirie kuanza upya maombi na hakuacha tena mpaka leo.


Mwanangu David nayeye alikuwa ananitafuta sana iliapate kunijua mama yake mzazi, wakati akiwa na miaka 30 alianza kunitafuta kwa udi na uvumba kazi ambayo haikuwa rahisi, ambapo ilimchukua miezi kupata cheti halisi cha kuasiliwa kwake(adoption) pamoja na cheti chake cha kuzaliwa na kuanza kunitafuta tena kwa bidii sana bila kuchoka. Wakati huo nami nilikuwa mgonjwa mgonjwa na kufanikiwa kuolewa uzeeni lakini nikawa kwenye shida tena baada ya ndoa yangu kuvunjika pamoja na hayo yote bado nilikuwa naomba sana niweze kukutana na mwanangu kwa mara nyingine "anasimulia Teresa

Teresa amesema alipofikisha miaka 70 alifikiria kwamba atakufa bila maombi yake ya kumuona mwanae kujibiwa. Mwaka 2008 mdogo wake wa kike alifariki dunia kitendo ambacho kilimfanya amuulize Mungu kwanini hakufa yeye badala ya mdogo wake kwasababu alikuwa na watoto pamoja na wajukuu wakati yeye hakuwa nao. Teresa anasema inawezekana kifo cha mdogo wake kilisababisha Mungu kumsikia kwasababu ndani ya miezi miwili ustawi wa jamii walimwambia mtoto wake anamtafuta akiwa tayari amemaliza miaka 20 katika kazi hiyo ya kumtafuta.

Nilikutana na mwanangu David siku ya Ijumaa kuu mwaka 2009 nilipata furaha ya ajabu kugundua pia nimebarikiwa kuwa na mjukuu wa kike kwa mwanangu, miaka yangu ya maombi hatimaye ikawa imejibiwa na sasa maombi yangu ni ya shukrani kwa Mungu, kwasasa naishi nyumba moja na mwanangu ambaye anataka niwe chini ya uangalizi wake jambo ambalo analifanya na kunipa matunzo mazuri na kusema sasa tutakuwa pamoja milele. Mimi na mwanangu wote ni wa imani moja, tunahudhuria kanisani pamoja najisikia fahari kuwa naye.

Teresa ameeleza kwamba mtoto wake alikuwa akilelewa katika familia ya Kikristo na alikuwa akipendwa sana na familia yake na wakampa maisha mazuri, hata yeye sasa amekuwa rafiki mkubwa na familia hiyo iliyomlea mwanae, ambao kwa pamoja wamemkaribisha katika familia yao pia familia hiyo imefurahi kuona Teresa ameungana na mwanae tena.

Najua Mungu amekuwa pamoja nami kwa miaka yote hiyo, akinilinda na kuniongoza na hatimaye kuonana na mwanangu, pamoja na kuwa hospitali kwa miezi kadhaa nikipata matibabu ya ugonjwa wa kifua kikuu(TB) mwanzoni mwa miaka 1960 pamoja na upasuaji mkubwa kutokana na ugonjwa wa saratani mwaka 2003, nimemwamini Mungu. Mwaka 2004 nilibatizwa na kuwa mfuasi wa Yesu kamili. amesema Teresa Pullman's akizungumza na gazeti la Good News.

Comments