MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

PICHA ZA IBADA YA JUMAPILI KANISA LA YESU KRISTO LA HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI KWA NABII FLORA PETER


Jumapili hii ilikuwa ni ya kipekee. Mungun aliweza kutembea kwa kila mmoja. Wingu lilitanda katika kanisa hili. watu walionekana kububujika kutoka na uwepo wa Mungu ulikuwepo mahali hapa. Ninaomba tushirikiane kwa kupitiam picha hizi
Nabii Flora (kushoto) na Msaidizi Mchungaji Jury

Jina la kanisa: Kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji
Eneo: Mbezi Salasala
Kituo: Shuka kituo cha Mbezi Mbuyuni barabara ya kuelekea Tegeta
Jina maarufu: Ukifika uliza Kanisa la nabii Flora
Simu: Nabii Flora Peter: +255 65744699 Octavian: +255716 310661
Blogu: www.nabiiflora.blogspot.com
Facebook: Nabii Flora Peter
Youtube: www.youtube.com/Nabii Flora Peter

Mpiga Picha wetu: Rumafrica Simu yake
Simu:+255 715851523
Blogu www.rumaafrica.blogspot.com au www.rumaafricajobs.blogspot.com
Dada huyu alikuwa na tatizo la moyo kutanuka na miguu, alipofika kwa nabii Flora aliombewa na sasa anasema hajisikii tena maumivu ya moyo bali miguu. Mungu anazidi kumponya.

Dada huyu ni mkazi wa Dodoma aliyekuja kwa Nabii Flora akiwa na tatizo la kuvimba mguu. Mguu huu ulikuwa na uvimbe mkubwa zaidi ya hapo. Nabii Flora alimuombea na sasa uvimbe unapungua. Mungu ni mwema.

Mama aliyefunga safari kutoka Songea mpaka Dar es Salaam kwa nabii Flora kwa kutka Nabii Flora amuombee mwanae aliyekuwa kiwete na hawezi kutembea kutoka na miguu kujikunja. Baada ya maombezi miguu ilijikunjua na sasa anasimama

Mwigizaji wa Luniga akishuhudia matendo makuu ya Mungu baada ya kuombewa na nabii Flora. anasema biashara zake zinaenda vizuri kabisa. Hapo mwanzo alikuja kwa nabii Flora akiwa amechoka kifedha.

Mama huyu akionyesha alama ya tick iliyotokea katika mkono wake baada ya Nabii Flora kutamka na kutabiri kuwa kuna watu watawekewa alama ya tick katika mikono yao kama ishara ya kukubaliwa na Mungu katika mahitaji yao.

Nabii Flora akiwa amempakata mtoto aliyekuwa akiumwa ugonjwa wa kuanguka kifafa na usiku kuzimia. Kulia ni mama wa huyu mtoto aliyemleta kwa Nabii Flora na kuombewa na sasa ni mzima hana kifafa na hazimii usiku.

Watu wakiwa wameangushwa kwa Nguvu za Mungu wakati Nabii Flora akiomba na kukemea mapepo

Nabii Flora akiwaombea watu wenye mangonjwa mbalimbali ambapo aliwaomba washike sehemu ya kutolea damu.Nabii Flora akiombea watu na kukemea mapepo

Kipindi cha kuombea wale waliofika madhabahuni kumtolea Mungu mafungu ya kumi.

Watu wakiwa wamedondoshwa na nguvu za Mungu baada ya Nabii Flora kuhesabu mara tatu

Nabii Flora akiwa kaika maombezi

Nguvu ya Mungu ikifanya kazi kwa kupitia mtumishi wake Nabii Flora Peter.

Watu wakiwa wametoka katika viti vyao na kusimama koridoni kwaajili ya kupokea baraka za Mungu kwa kupitia mtumishi wake nabii Flora Peter.Nabii Flora Peter akiwa amesimama juu ya kiti akimwaombea watu, na hii ni kutokana na watu kutomuona hasa waliokaa nyuma.
Kwaya Kuu ya hapa kanisani.Apostle Gideon Mutalemwa akiongoza sifa

Mtumishi wa Mungu cameraman Octavian
0