RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWIMBAJI GRACE RWEGASHA AWEKA WAZI MAOVU YA WATUMISHI WA MUNGU, WAIMBAJI WAPENDA PESA, KUVUNJIKA KWA NDOA ZA WAIMBAJI, MAOVU YANAYOFANYIKA STUDIO N.K


Huyu ni mwimbaji wa kipekee katika waimbaji niliowahi kufanya nao mahojiano na amekuwa muwazi juu ya maovu yanayoendelea kwa tumishi wa Mungu na pia ameweza kuwashauri na kuwaonya kuwa vitendo hivyo sio vizuri kwa JICHO LA MUNGU LINAONA KILA MAHALI NA HUWEZI KUJIFICHA NA IPO SIKU MUNGU ATAKUANIKA MBELE ZA WATU. Maneno haya ni magumu sana na yenye nguvu ya ajabu kwa yule anayeelewa na kujali. Grace na Joshu wanamtumikia Mungu kwa kuimba na Mungu amewapa uwezo wa kuimba kwa kutumia lugha mbili yaani Kiingereza na Kiswahili, uimbaji wao ni wa tofauti sana ukifananisha na waimbaji wengine.

Ukimsikiliza sana huyu dada Grace kwa makini utaamini ya kwamba mbali ya uimbaji Mungu amempa karama nyingine ya kiuchungaji kutoka na upangiliaji wake wa maneno anapoongea na jinsi anavyolijua Neno. Waimbaji wakiweza kumtumia vizuri mwimbaji huyu kwa ushauri hakika watafika mbali kwani kuna kitu anacho ndani yake cha kipekee sana.

Hivi sasa ameweza kufanikisha kumaliza albamu yake ya MY SAVIOUR GOD akiwa na mdogo wake Joshua (Joshu) na kikundi chao kinaitwa GRACE AND JOSHU

Unaweza kuwasiliana naye kwa simu hizi +255 788 443 346


Comments