RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RAIS WA CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI TANZANIA, ADDO NONEMBER ASHIRIKI KATIKA MZIBA WA MWIMBAJI MKONGWE MAREHEMU NGURUMO NYUMBANI KWAKE SIKU YA JANA

Huu ni moyo wa upendo aliouonyesha mwimbaji na rais wa CHAMUITA kwa kuungana na wafiwa wa marehemu Ngurumo katika kuomboleza siku ya Jumatatu. Addo Novemba aliyevalia kote nyeusi katika picha akiwa katika harakati za kusaidia shughuli zinazoendelea nyumbani hapa kwa Marehemu Mzee Ngurumo. Mungu na azidi kuwafariji wafiwa..Amina

Mwanamuziki mpapasa kinanda, Abdul Salvado ‘Father Kidevu’ akisalimiana na mwakilishi wa Global.

Wawakilishi wa Global Publishers, Sifael Paul (anayeandika kwenye daftari) na Elvan Stambuli mwenye kizibao, wakiandika mchango wa Kampuni ambao ni shilingi 500,000 kabla ya kuwakabidhi ndugu wa marehemu Muhidini Gurumo leo jioni nyumbani kwa marehemu Makubuli, Dar, leo. Atazikwa kesho Masaki, Kisarawe.


Mwakilishi wa Global Publishers, Elvan Stambuli akimkabidhi mjomba wa marehemu Muhidini Gurumo, Yahya Mikole (katikati) shilingi 500,000 ambazo ni rambirambi ya kampuni kwa msiba huo.


…Fedha zikihesabiwa.


Mwakilishi wa Global akizungumza, Stambuli akimtambulisha Mhariri wa Ijumaa Wikienda, Sifael Paul kwa nguli wa muziki King Kikii ambaye alikuwepo msibani leo.



Hawa ni wadau wa muziki wa dansi wakiwa msibani keo huku wakionesha sura za huzuni.
Rashidi Pembe (mpuliza saksafoni kulia) akiwa na King Kikii msibani leo.

Comments