RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SEMINA MKOANI IRINGA KWA ASKOFU BOAZ SOLLO YAPAMBWA NA MWIMBAJI YELONIMO MWALO NA ANNA DAT SIKU YA LEO

Mbali na kupata Neno la Mungu kutoka kwa Askofu Boaz Sollo wa kanisa la Overcomers Power la Iringa na mgeni wake kutoka Dar es Salaam, Profesa Pius Ikongo ambao walihubiri injili ya Yesu na kuwafungua watu waliofungwa na shetani na kutumikishwa kwa muda mrefu, mwimbaji Yelonimo Mwalo na Anna Dati kutoka Arushawalikongo mioyo ya watu pale Mungu alivyowatumia katika huduma yao ya uimbaji. Watu wa Iringa waliwapokea kwa vifijo na nderemo hasa pale walipotoa sauti zao nyororo zenye kumgusa Mungu kwa uimbaji.

Wanakwaya ya agape wakimsindikiza bwana mwalo wakati akimtukuza bwana.


Semina hii imedumu kwa takribani siku thelathini ambapo siku ya leo watu walikuwa wemgi sana waliofika kusikiliza Neno la Mungu kwa kupoitia watumishi wa Mungu, Askofu Boaz na Profesa Ikongo.  Semina hii inamalizikika siku ya Pasaka.

Anna Dat kutoka Moshi akimsifu mungu katika semina hiyo.

Yelonimo Mwalo mume wa mwimbaji wa nyimbo za injli Stera Joel akimsifu mungu katika semina hiyo.



Comments