RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWENDELEZO WA MBEYA GOSPEL FESTIVAL 2014 CHINI YA CHAMA CHA MUZIKI TANZANIA

Chama cha Muziki wa Injili Tanzania chazidi kufanya makubwa mkoani Mbeya. Wanambeya wapokea kitu ambacho hawajawahi kukipokea tangia Mbeya imeitwa Mbeya nikimaanisha haijawahi kutokea hata siku moja CHAMUITA kufanya tamasha kubwa kama hili mkoani Mbeya. Hii ni bahati kwa wakazi wa Mbeya, wanatakiwa kutambua ya kwamba Mungu anataka wakazi wa Mbeya wote kuokoka na kumtumikia Mungu. Wakazi wa Mbeya ni watu wenye karama ya uimbaji ambayo Mungu ameweka ndani yao, sasa umefika wakati wa kumuimbia Mungu na kumtukuza.

CHAMUITA imekuja kwenu ili muweze kujiunga na hiki chama ambacho kimekuwa msaada mkubwa sana kutetea haki za waimbaji Tanzania. Waimbaji wamekuwa hawanufaiki na huduma yao ya uimbaji, wamebaki kuibiwa na kudhurumiwa na mwisho wa siku wanaishia kuwa maskini hata kama wanafanya kazi ya Mungu, wameshindwa kutambua haki zao za kimuziki. Lakini leo Mungu ameweza kutumia watu wake kwa kupitia CHAMUITA kuwakomboa waimbaji hawa wenye nia ya kumuimbia Mungu lakini wanabaki maskini wakati wanamtumikia Mungu ambaye ni tajiri duniani na mbinguni.

Kama mwimbaji wa nyimbo za injili unashauriwa kujiunga na hiki Chama ili kikusaidie katika kuboresha huduma yako ya uimbaji na kuhakikisha unapata haki zako zote unazostahili kuzipata kwa kupitia huduma yako ya uimbaji. Tumechoka waimbaji kudhurumiwa na kuonewa na watu wa dunia hii ambao hawana hofu ya Mungu, wamebaki kutunyanyasa na kutuchoma na miimba mikali katika miili yetu.

Mungu akusaidie ili utambue umuhimu wa kujiunga na chama hiki pekee Tanzania chenye kutetea na kumlinda mwanamuziki wa injili. Tuone baadhi ya matukio yaliotokea mkoani Mbeya hivi karibuni.

Weni katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS


John Shabani na mwanamama Rachel sharp kutoka Sweden

Masanja akimkaribisha mkuu wa wilaya

Masanja, Ammy mwakitalu na John Shabani
Watu wakikata shauri






ANGALIA MATUKIO MENGINE KWA KU-CLICK Read More HAPO CHINI



Mamia waokolewa


Baada ya siku mbili nje, sasa Mbeya gospel festival ikiwa inasubiriwa kwa hamu na wakazi wa mbeya ndani ya ukumbi wa mtenda sunset.....!!

Meza kuu ikiwa inaendelea kutafakali ndani ya mbeya gospel festival..kushoto ni John Shabani, katibu mkuu wa chama cha muziki wa injili Tanzania katikati ni mkuu wa wilaya ndugu Noman Sigalla na kulia ni Mh. Luvanda (Diwani – Njombe) mwenyekiti wa mipango wa chama

Comments