RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWANAMKE ALIYEASI UISLAMU ASAFIRISHWA KWENDA ITALIA


Meriam Ibrahim akiwa na mumewe Daniel Wani pamoja na mtoto wao wa kwanza.

MWANAMKE wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa kuasi dini ya Kiislamu na kuolewa na Mkristo, Meriam Ibrahim, amesafirishwa kuelekea Italia baada ya kukaa ubalozi wa Marekani mjini Khartoum, Sudan kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Meriam na familia yake wameondoka na ndege ya Serikali ya Italia wakisindikizwa na Makamu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Lapo Pistelli.

Awali Meriam alihukumiwa kifo na viboko 100 baada ya kuasi dini ya baba yake ambaye ni Muislamu na kuolewa na Mkristo, Daniel Wani.

Baadaye mwanamke huyo alifanikiwa kuachiwa huru baada ya wanaharakati kuingilia kati japo alikamatwa tena kabla ya kuachiwa na kukaa katika ubalozi wa Marekani, Khartoum.

Comments