RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PICHA ZA AWALI MAZISHI YA MAMA MCHUNGAJI ORIDA NJOLE

Hakika kila jambo lina mwanzo na mwisho. Kama binadamu lazima utambue hilo kuwa ipo siku utazikwa na je kama ukizikwa unajua ni wapi unaelekea? Marehemu mama mchungaji Orida Njole kama vile alijua na ndio maana aliamua kumuachia Mungu maisha yake na kuanza kumtumikia kwa njia ya uimbaji. Jiulize wewe unafanya nini kwa utukufu wa Mungu.

Marehemu mama mchungaji Orida Njole aliyefariki siku ya Jumamosi katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam pia alikuwa mama Mchungaji kwenye kanisa la 'Oasis of Victory Church', mume wake akiitwa Peter Simon - amezikwa kwenye makaburi ya mwisho wa lami, Kijiji cha Wagogo, Salasala, baada ya kumaliza ibada ya maazishi iliyofanyika Salasala Kwa Swai.



































KIPINDI AMELAZWA KATIKA HOPITALI YA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM.
BONYEZA "Read More" HAPO CHINI  KUONA PICHA ZAKE



Kwa wale wasiomjua Oride Njole, ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Leo hii yuko kitandani anaumwa, anatamani kuwa kama wewe ambaye kwa sasa unacheka na kufurahi lakini anashindwa kutokana na ugonjwa alionao. Jamani ndugu yetu anaumwa sana tunapaswa kumuombea na ikiwezekana tufike pale hospitalini Temeke hospitali ya serikali.


Orida Njole

RUMAFRICA YAPATA TAARIFA ZA UGONJWA

Rumafrica imepokea habari hizi siku ya leo kwa njia ya simu kutoka kwa mtangazaji wa Radio Tumaini Obedi Kikao, anasema hali yake sio nzuri sana, ndugu yetu anateseka sana. Kama binadamu mwenye huruma basi fika pale hospitalini kumpa pole ndugu yetu huyu. Kumbuka ulikuwa naye kipindi mnacheka leo hii mwenzetu amenuna kutoka na maumivu anayopata. Anahitaji faraja kutoka kwako Mtanzania.



NDUGU NA MARAIKI
Kumbuka wewe rafiki uliyekuwa unacheza naye mpira wa mikono, Oride ni mwanamichezo mkubwa sana na amekuwa nawe katika michezo mbalimbali, lakini leo hii anashindwa hata kushika mpira kutoka na ugonjwa alionao. Umefika wakati wa kwenda kumuona ndugu yetu na kubwa zaidi ni maombezi.


WACHUNGAJI NA WATUMISHI WA MUNGU

Mchungaji ambaye ulikuwa ukimtumia Oride Njole katika huduma yako, ameimba sana kanisani kwako lakini leo hawezi kuimba tena kutoka na kile kinachomsumbua. Nenda basi ukamuombee pale kitandani alipolala ili aweze kuamka na kufanya kazi ya Mungu kama zamani. Kuwa na moyo wa huruma basi.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj0zCbKDfBmX9qFwIq44Mqb7e4SSe68uoFmcJsedWilX0VfGUh-EUNZ7NdUNpqBRsOPMDyRqarjnvTkfCZsxZq3gteBrxBE4HYOgOmi7KhlNrGzAbLQGyFr9ye6DmJcVcj0Zhu1wnjCuGA/s640/orida6.jpg
Orida Njole akimtumika Mungu kanisani

Hata wewe mchungaji ambaye unayemfajhamu na wewe uliyemfahamu kwa kupitia blogu hii ya Rumafrica basi acha hicho unachofanya sasa anza kumuombea. Ondoa hiyo roho inayokusukuma usimmuombee na ikemee sasa.

WANAMICHEZO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhhAG5cRoqgGNCjCRPCYaKhESAgArjR34Fo7nLA57Yxc_gHhKh1vdsaO2pI479Ovi38ggV410hVK8Z7KhXJ05YpgscpPPKk3XAkJNTUQ_N7Rpqklbqsbcnw1AH6T9coZibUxTQFwH8cfqc/s640/DSCN7837.JPG
Orida Njole (kushoto)

Marafiki zake ambao mmekuwa naye studi kurekodi nyimbo za kumtukuza Mungu, sasa tunawaomba mfanye maombi na kufika pale hospitalini kumtia moyo na kumpa pole. Mmekuwa mkicheka na kupeana mawazo studio lakini leo hii mwenzenu anashindwa hata kuwapa mawazo kutokana na maumivu anayopata. Kuwa na moyo wa upendo na huruma kama vile mnavyotuimbia sisi tuyafanye yale manyoimba.
http://photos-a.ak.fbcdn.net/hphotos-ak-ash3/t1.0-0/c0.2.960.639/s720x720/379618_192151074260838_1925803444_n.jpg
Orida Njole kushoto wa kwanza
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgXOmc_6ApM9IjPksw8RMrH8jToXXc_-80IITtO7DBQ_f9XWew1YfCS44rZnGHhwIb4zx_xsPstID43E1Keru9DbO1t_DjXgDfO827F-EHR_cco2_gBY8drrKYxExoNz1qtPouDE0H7eVyS/s640/Orida-Njole-Poster.jpg
DVD Cover la albamu ya Orida Njole

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjm1I_44NPimgC52i_623YN_1xT2YtvsloGQVIvCHlIa1nrELYrt0Y_7r34F9XXqXIMRseTiBA-UmIl_poSYaK_eqlXNBlws3S07thsrLZhG-_kaqPfaH4RE5x1k-uqkSJWLeSdjipF0hba/s640/Orida.jpg
Orida Njole

Comments