RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA INAPINGA KILE KILICHOSEMWA NA WAKAZI WA IRINGA YA KUWA FLORA MBASHA AIMBE BONGO FLEVA NA SIO INJILI TENA

Rumafrica inapinga kili kilichosemwa na baadhi ya wakazi wa mkoa wa Iringa ya kwamba Flora Mbasha sasa aachane na uimbaji wa nyimbo za Injili na badala yake aimbe Bongo Fleva. Kwanini wakazi hawa wanasema hivyo? Inasikitisha sana...

Flora Mbasha amemtumikia Mungu kwa muda mrefu sana. Watu wameokoka wengi kwa kupitia uimbaji wake. Watu wamemjua Yesu Kristo kwa kupitia huyu dada Flora Mbasha. Mwanamuziki huyu mbali na kumtumikia Mungu, hajawahi kupata skendo yoyote mbaya maisha mwake, amependwa sana na wananchi walio wengi. Taoifa la Tanzania limetokea kumpenda sana na kumwamini hata kuimba nyimbo za kulisifu Taifa la Tanzania. Viongozi mbalimbali wamemtumia sana katika kulitumikia Taifa hili la Tanzania kwa jia ya uimbaji.

Flora Mbasha na mume wake Emmanuel Mbasha wamekuwa mfano mzuri sana katika maisha yao ya ndoa kwa kupendana na kushirikiana katika uimbaji wao. Tumeona wakisaidia jamii kwa misaada mbalimbali.

Leo hii limetokea hili linaloimbwa katika vinywa vya walio wengi kuhusiana na Emmanuel Mbasha kumbaka shemeji wake. Mema yote yamefutwa na hawa waliokuwa wakimpenda Flora Mbasha na mumewe na kuanikwa hadharani hili ovu moja tu...Jamani hii sio haki kabisa, kumbukeni na mema aliyoyanya mtumishi huyu wa Mungu. Kumbukeni ya kwamba Mungu wetu wa mbinguni husamehe na ufuta dhambi zetu hata zikiwa nyekundu kama damu. Mungu wetu ni Mungu wa msamaha na huruma. Tusiwe watu wa kuhukumu na kukatisha tamaaa wakati bado tunaishi happa dunia. Leo limetokea kwa Flora Mbasha na mumwe wake kesho litakutokea. Shetani anafanya kazi usiku na mchana kuharibu kazi ya Mungu, ndugu zetu hawa walivamiwa na huyu shetani na nafsi zao zinajuta kwa kile kilichotokea.

Mungu wetu aliweka kiti kinaitwa TOBA, mtu anapokosea ni lazima aungame dhambi zake na kukiri kuwa ni kweli alifanya na anahitaji kusamehewa na Mungu. Sasa wewe unayemuhukumu Flora Mbasha unajuaje pengine ameshatubu mbele za Mungu na kusamehewa dhambi zake. Mungu wetu hapendi kabisa kuona mwanadamu anamhukumu mwanadamu mwezake kwani yeye hana mamlaka hayo chini ya jua.

Enyi wakazi wa mkoa wa Iringa mliyetamka maneno ya kukatisha kazi ya Mungu kwa kupitia huduma ya uimbaji ya Flora Mbasha na mume wake kutubu dhambi hiyo kwani haipendezi kabisa.

Ewe mdau wa blogu hii, soma kile kilichoandikwa na blogu ya Francis Godwin ikielezea kile kilicholalamikiwa na wakazi wa mkoa wa Iringa kuhusiana na Flora Mbasha

WADAU WA MUZIKI WA INJILI IRINGA WAMCHOKA FLORA MBASHA WAMTAKA AIMBE MUZIKI WA BONGO FLEVER SIO INJILI TENA

ZIKIWA zimepita siku chache toka kumalizika kwa sakata la mume wa Flora Mbasha kutuhumiwa kumbaka shemeji yake na Flora Mbasha kuhusishwa katika mchezo huo ,baadhi ya wadau wa mwimbaji huyo mkoani Iringa wamempa ushauri wa bure mwimbaji huyo kuwa kwa sasa ni vema akakaa kando na uimbaji wa nyimbo za injili na badala yake kujikita na uimbaji wa muziki wa bongo Flever

Wakizungumza mtandao huu wadau hao Hosea Kalinga na Neema John walisema kuwa heshima kubwa ambayo msanii huyo alikuwa ameipata imeporomoka kwa kasi kubwa kufuatia matukio mabaya yaliyoikumba familia yake na hivyo hata kama waandaaji wa matamasha ya injili watamwalika mwimbaji huyo ni wazi wanaweza kuambulia patupu kutokana na kupotea ghafla katika mionyo ya watu .

"Tulikuwa tukimkubali sana Flora Mbasha na Mumewe enzi wakiimba pamoja ila kwa matukio haya ya kidunia ambayo yamewakuta hakuna mpenzi wa nyimbo za injili atakayempenda mwimbaji huyo na nyimbo zake ni vema akatafuta soko la uimbaji katika miziki ya dunia kama bongo Flever na sio injili tena"

Kuanza kubezwa kwa mwimbaji huyo kumekuja kufuatia mgogolo wa ndoa yake ulioibuka kutokana na sakata la mume wake kudaiwa kumbaka shemeji yake huyo Flora Mbasha akidaiwa kuwa na mahusiano na mmoja kati ya wahubiri wakubwa hapa nchini .

Comments