RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SAFARI YA MWISHO YA MWANAMUZIKI WA LIFE BAND ARUSHA BWANA EGLAH BAVUMA YATIMIA

Hii inatukumbusha ya kwamba kila jambo chini ya jua lina mwanzo na mwisho. Unaweza kujiona kama vile hutakufa lakini tambua ipo siku utakufa. Leo hii ndugu yetu hakujua kuwa siku ya leo atakuwa katika sanduku akipelekwa kuzikwa. Yamkini alikuwa na mipango mingi sana ya mwaka huu 2014, lakini haijafanyika na Mungu ameamua kumchukua.


Kitu cha msingi alichokionyesha wakati wa uhai wake ni pale tu alipoamua kuokoka na kumtumikia Mungu kwa njia wa muziki wa Injili. Kuna baadhi ya watu wameokoka au kuguswa na nguvu za Mungu kwa njia moja au nyingine kwa kupitia huduma yake hii ya muziki.

Sisi tuliobaki tunahitaji sasa kumtumikia Mungu na kuachana na dhambi kwani zitatupeleka jehanamu. Tuache kuwa na wokovu wa fashion ili kuficha maovu yetu, kwani tukifanya hivyo Mungu wetu wa mbinguni atatutapika na kutufukia na mchanga, tutaonekana kinyaa kwake.

Leo hii utajifanya umeshikwa na uchungu wa ndugu yetu lakini baada ya muda fulani utamsahau na utaanza kurudi nyuma na kufanya maovu. Uchungu ulionao kwa ndugu yetu aliyetutangulia ubaki kuwepo maishani mwako siku zote. Hiyo hofu ulioyonayo ya kumuogopa Mungu na kumheshimu kutokana na msiba huu  sasa iendelee kuwepo hadi pale Mungu atakapokuita.

Mimi na wewe tunahitajiana na tuombeane ili tusirudi nyuma, tusonge mbele kama ndugu yetu alivyosonga mbele kwa kumtumikia Mungu mpaka mauti inamfikia.

Wenu katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS
+255 715 85 15 23



Comments