RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SIKU NILIYOFAHAMIANA NA MAREHEMU ORIDA NJOLE - RULEA SANGA

NILIVYOKUTANA NAYE MAREHEMU ORIDA  NJOLE
Orida Njole kwa mara ya kwanza, nilimjua kwa njia ya Facebook. Nakumbuka siku moja nilikuwa nachati katika facebook, nikaona ameni-request (ameniomba) niwe rafiki, nilimkubali na akawa rafiki kama marafiki wengine katika facebook.

Baada ya kuangalia profile yangu katika facebook, alipendezwa sana na kazi zangu za Graphics na kuniomba nimtengeneze kava la albamu yake ya "Duniani Tuwapitaji" Pia alivutiwa sana na safari angu ya Nigeria na akanipigia simu ili apate kujua mengi kuhusina na mtumishi wa Mungu Nabii TB Joshua. Nilimpangia siku ya kuja ofisini kwangu Sinza Afrikasana hapa Dar.

KUTENGENEZA KAVA LA ALBAMU YAKE
Pia marehemu Orida Njole alitaka nimtengenezee kava la albamu yake ya "Duniani Tuwapitaji", niliweza kumtengenezea na ninakumbuka siku hiyo alikuwa katika furaha sana. Orida Njolea kabla ya kutengeneza kava lake la albamu yake aliomba ushauri wa nguo za kuvaa na mimi nikamwambia ni vizuri kuvaa ngu za kitenge, naye alijibu na kusema "Kama ulijua hivi, na mimi nilitamani kuvaa nguo hizo ili nionyshe Utanzania wangu"

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi_svQsJpseJC6DBztLdm49QrRk_0TpwVUfEcefs4M8SNNpfntIBDhqu1oBJbgfQZcynO1ncz6N8yoj_xpUaFiioeNV4dWHXtFOAgVL8Ba5mZ6fn_aEu_PwdTK9ubNHjm258y4F7VJblpIz/s640/Orida-Njole-CD-Cover-Paper+A.jpg
 Baada ya kutengeneza hilo kava hapo juu, naona hakupendezewa na akaamua kumtumia mtu mwingine na kutengeneza kava hili hapa chini ambalo linatumia sasa hivi.

MAHOJIANO KATI MAREHEMU ORIDA NJOLE NA RULEA SANGA
Baada ya kumaliza kumtengezea kava lake aliomba nifanye naye interview, nami nilimkubali na tukafanya naye Interview ambayo utaisikia hapo chini.

SIKILIZA MAHOJIANO HAYA

ALITAMANI KUJUA HISTORIA YANGU
Nakumbuka siku moja aliniuliza, wapi ninatokea nami nilimweleza kuwa natokea mkoa wa Iringa, Marehemu Orida Njole alifurahi sana kwani na yeye alikuwa anatokea mkoa wa Iringa. Hii ilifanya mahusiano yetu kuwa ya karibu sana na tuliishi kama ndugu tukishauriana na kutia nguvu kwa kazi ya Mungu. marehemu Orida Njole alikuwa ni mtu wa kupenda sana kucheka na kuchangia maada mbalimbali.

KIPINDI CHA HARUSI YA STELLA JOEL
Siku ya harusi ya Stella Joel nakumbuka aliweza kuniambia kuwa anatamani sana kuolewa, anapenda siku moja aolewe na mtumishi wa Mungu. Mimi nilimtia moyo na kumwambia Mungu wetu ni Mungu anayesikiliza sauti za watumishi wake, na wewe ni mtumishi wake, ipo siku atatimiza haja ya moyo wako.

VITU ALIVYOVIPENDA SANA
Marehemu Orida Njole aliniambia katiika vitu anavipenda sana ni michezo na hasa mpira wa mikono (netball). Tuone baadhi ya picha alizozileta Rumafrica
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEglm876OSHyMTq28XQdHgOA_H3xlswrahYF7kycz1ogSmuYayyTXBAm4_1j0I6s_Wa96Lhr_SGq3b3SjFtCGe9ZFUCocHF-raoTkZHvDaRLb1kElfW9XlHdsgKTfZTeqXVimdbXfAmLTPOW/s640/DSC_0061.JPG
Kushoto ni marehemu Orida Njole enzi za uhai wake

Kulia ni Marehemu Orida Njole akiwahi mpira enzi za uhai wake
Bonyeza hapa kuona picha zake za michezoni

Orida Njole alipenda sana kitimoto kama unavyomuona akiwa na baadhi ya watangazaji wa Praise Power na Clouds FM wakikivamia kitimoto (nyama ya nguruwe). Katika picha ya hapo chini alikuwa Afrikasana Sinza katika harusi ya Stella Joel, wakimsubiria Stella Joel kutoka saluni alikokuwa akipambwa.

http://3.bp.blogspot.com/-5ClYn0TMNyA/U8OS4zfUOTI/AAAAAAAAAvQ/Ohml3yru9x4/s1600/dddd.jpg
Wa tatu kuliwa ni Marehemu Orida Njole
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEisLQeUT2MoLQ_K1g-OqZNGiJmgVMjRFh03PYCvmxU2O5JG7im9bV_mjFwE17leyKewtvcu_g8hTr64glmSP6be2nSoszSYg5YxKkj6Jfjma9FnI12V-BRACUbKG60e9xRqdpMnkH3Vwag/s640/DSCN7671.JPG
Stella Joel akiwa katika maandalizi harusi yake

Marehemu Orida Njole nyuma ya bibi harusi Stella Joel wakitoka Saluni Dage's wakielekea kanisani
Kulia ni Marehemu Orida Njole kanisani

Kushoto ni marehemu Orida Njole

KIPINDI CHA KUCHUMBIWA
Marehemu Orida Njole aliweza kunitaarifu kwa njia ya simu ya kwamba amempata mchumba ambaye ni mtumishi wa Mungu na wamependa sana. Mahusiano yao yaliendelea mpaka wakafunga ndoa. Ninasikitika sana siku ya harusi yake si kwenda na sijui ni kwanini?
Baada ya kumaliza harusi yake aliweza kunitaarifu na kumshukuru Mungu kwa kumtimizia haja ya moyo wake. Alisema' " Ninafuraha sana ndani ya Moyo wangu, kwani nimempata yule niliyekuwa namtafuta kwa muda mrefu sana"

KIPINDI CHA UGONJWA WAKE
Kipindi chote cha ugonjwa wake, nilikuwa sijui kabisa kama anaumwa. Siku moja akanipigia simu na kusema "Rulea mwenzio naumwa sana, nimekonda sana, naumwa rafiki yangu, kwani ulikuwa hujui?" Nilisikitika sana alivyoniambia, nikamjibu,
Wa pili kutoka kulia ni Orida Njole wakati wa enzi zake akisubiria mwili wa marehemu Debora Said kushushwa katika gari.


"Nilikuwa sijui kama unaumwa, pole sana, nitakuja kukuona rafiki yangu" Baada ya siku chache ulitokea msiba wa Mchungaji Debora Said wa kanisa la Maisha ya Ushindi Ubungo External - DSM, nilihudhuria ule msiba.
Aliyevalia tshirt nyeusi imeandikwa GOD ni marehemu Orida Njole katika msiba wa Mch. Debora Said Ubungo


Nikiwa msibani nikipiga picha Marehemu Orida Njole aliniita, nami nilipogeuka nikamuona akiwa amepungua sana, nilishangaa sana na kujua kweli dada yangu Orida Njole alikuwa anaumwa. Nilimuona akiwa hana nguvu za kutosha, midomo yake ikiwa imekauka, nilisikitika sana.

Orida Njole aliomba sana nimpige picha, nami nilimpiga na akanitania na kusema, "Hiyo mifupa utamuonyesha nani? Nilimtia moyo na kusema wala hujakonda sana...Marehemu Orida Njole alinisimulia historia ya ugonjwa wake, huku akionekana akitaka kulia, niliumia sana na kumuonea huruma sana rafiki yangu. Nikakumbuka maneno yake aliyoniambia ya kwamaba, "Rulea sasa unatakiwa kuoa maisha ni mafupi" Nikamuahidi marehemu Orida Njole kwamba nitakwenda nyumbani kwake kumuona, naye alifurahi sana na kusema kuna mengi atanisimulia.
Baada ya mazishi ya Debora Said kumalizika nikaambiwa Orida Njole alizidiwa sana na ikalazimika kupelekwa nyumbani kwake. Hazijapita siku chache nikapigiwa simu na Obed Kikao Mtangazaji wa Tumaini Radio ambaye alikuwa akipiga sana nyimbo marehemu Orida Njole redioni na akanambia Orida Njole anaumwa sana tena sana, niangalie kwenye facebook kwa Joshua Makondeko ka-post picha zake. Niliingia katika facebook na kuona picha zake, niliumia sana kumuona Orida akiwa katika hali ile. Nilimpigia simu Obed Kikao na kumuomba kwenda naye katika hiyo hospitali ya Temeke alikolazwa, Obedi akanambia twende siku ya pili kwani muda ulikuwa umeenda sana. Ilipofika siku ya pili tukapanga kwenda kumuona jioni, hazikupita dakika nyingi nikapigiwa simu ya kutoka kwa Stella Joel na kuniambia Orida Njole amefariki dunia, nililia sana.

Nikiwa katika maandalizi ya kwenda msibani, nikapigiwa simu na Furaha Sanga na kuambiwa kuwa shemeji yangu Chaula amefariki dunia. Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwangu, ikanilazimu kufunga safari siku ya pili na kuelekea Mbeya kwa mazishi ya shemeji yangu. Kuanzia hapo sikuweza kuona tena ORIDA NJOLE

MAZISHI YA MAREHEMU ORIDA NJOLE
Baada ya kurudi mkoani Mbeya nilikoenda kumzika shemeji yangu nilifika Dar wakati mazishi yalishamaliziki. Tuone baadhi ya matukio katika mazishi ya marehemu Orida Njole

Ni kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kazi yake kwani haina makosa.

Comments