RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

UTHIBITISHO:WAUMINI 30 WA KANISA LA MORAVIAN KORTINI KWA VURUGU, SOMA HABARI ZAIDI HAPA

Kesi namba inayowakabili waumini hao. Na Haruni Sanchawa na Gabriel Ng’osha/GPL
WAUMINI wapatao 30 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni leo jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hadharani katika Kanisa la Moravian lililopo Mwananyamala-Msisiri ” A” Wilaya ya Kionondoni.

Katika kesi hiyo iliyounguruma kwa muda wa saa mbilli imeelezwa kuwa Julai 20 mwaka huu katika kanisa hilo lililopo eneo la Mwananyamala Msisiri ‘A’ waumini hao kwa pamoja walifanya fujo zilizosababisha kuhatarisha amani.

Kesi hiyo iliyosomwa na mwendesha mashitaka wa serikali, Credo Rugajo mbele hakimu mwandamizi wa mahakama hiyo Boniphace Lihamwike, ilidaiwa kuwa Julai 20 waumini walianzisha mzozo uliosababisha waumini kupigana na kusababaisha askari polisi kutumia nguvu kubwa kutuliza fujo hizo ikiwa ni pamoja na kutumia mabomu ya machozi.

Baada ya kusikiliza kesi pande zote mbili, Hakimu Lihamwike alisema dhamana iko wazi kwa kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja anayeaminika na shilingi milioni moja kimaandishi kwa kila mmoja.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 4 mwaka huu itakaposikilkizwa katika mahakama hiyo.

Hii ni safari ya kwenda kusomewa mashitaka yao.
Akina mama wakificha sura zao baada ya kutoka mahakamani.
Watuhumiwa wakiingizwa mahakamani.
Wakitoka kusomewa mashitaka.
Wakili Henzron Mwakenja akipokea hati ya dhamana kwa watuhumiwa.
Waumini wa kanisa la Moravian wakificha sura zao wakati wa kuingia mahakamani.
Kundi la kwanza la waumini waliokuwa wanasali nje Hili ndilo kundi la pili la waumini waliokuwa wanasali ndani.

Askari wakiwa eneo la mahakamani.

Baadhi ya ndugu na waumini wa Moravian wakiwa nje ya geti la mahakama.



Majina na nyaraka ya watuhumiwa wa vurugu za kanisa la Moravian.



Comments