RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EMMANUEL MBASHA NDANI YA STUDIO AKIFANYA YAKE HATA KAMA YUKO KATIKA MAPITO MAKALI

Hata kama mapito yako mbele yako lakini maisha lazima yaendelee. Emmanuel Mbasha ambaye oyuko katika wakati mgumu sana kwa kosa la kubaka na mke wake kutoweka ndani ya nyumba yao, bado mwimbaji huyu anapambana na maisha. Huwezi kukaa kimia eti unapitia mapito magumu, inakupasa kusonga mbele kulizungusha guruduma ili lisonge mbele. Tunajua kila mtu ana lake analopitia na bado anafanya kweli kuhakikisha kinywa kinapata msosi.


Emmanuel Mbasha mume wa Flora Mbasha

Kutoka na huyu ndugu yetu tunajifunza mengi sana lakini kubwa zaidi nililoona ni kwamba kutokata tamaa hata kama huko katika wakati mgumu sana, unapasa kuangalia mbele na kutotzama nyuma kwani ulikotoka ni kubaya zaidi kuliko kule unakokwenda (MAISHA LAZIMA YAENDELEE)

Hawa ndugu zetu wanahitaji sana kuwaombea ili wazidi kumtumikia Mungu kwani kuna mamzuri mengi wamefanya na tunatakiwa kuyakumbuka na kuwaombea. Kila binadamu ana udhaifu wake na hakuna binadamu mtakatifu chini ya jua, wote tunaishi kwa neema ya Munguu tu.

Watumishi wa Mungu tunatakiwa kutambua mchango wa hawa ndugu zetu na kuuthamini, tuwakumbuke katika kipindi hiki kigumu, jamii tuwapokee hawa ndugu zetu na kuwaunga mkono, kanisa lishikamane kuwaombea ili warudi katika mstari wao wa zamani. Kuna faida gani kwako mchungaji au mtumishi wa Mungu unapoona kondoo wako anapotea.

Mimi nisiwachoshe ngoja niendelee na yangu na kuwaombea hawa jamaa na ndugu zetu.

Wako katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS








Comments