RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EXCLUSIVE: MWIMBAJI MACHACHARI TANZANIA YELONIMO MWALO KATUPIA NYIMBO ZAKE YOUTUBE SIKU YA LEO

Yelonimo Mwalo ni mwimbaji anayekuja juu sana kwa kazi ya Mungu, siku ya leo ameweza kufanikiwa kutupia nyimbo zake youtube ili wewe na mimi tupate kusikia ujumbe wa Mungu. Kazi anayofanya huyu mwimbaji ni ajabu sana kwa kupitia uimbaji wake mzuri na jinsi Mungu alivyomjali.


Yelonimo Mwalo


Hakika Mungu wetu atabaki kuitwa Mungu kwani anajua vichwa vya kuviinua kwa kazi yake na pia anaangalia wale walio tayari kwa kazi yake. Yelonimo baada ya kuguswa na uwepo wa Mungu alisukumwa mpaka studio na kurekodi albamu yake ya Hatuwezi bila Mungu. Unaweza ukajiuliza alikuwa na maana gani ya kusema Hatuwezi Bila Ya Mungu, nafahamu yeye ana maana yake, na ukisikiliza wimbo huu utajua alikuwa na maana gani.


Yelonimo Mwalo audio CD Cover

Rumafrica kama kawaida yake inajipanga kukutana na huyu mwimbaji ili atuelezee juu ya albamu yake hii ambayo imetokea kupendwa na walio wengi sana kutoka na ujumbe aliouimba. Unaweza kuwasilina na huyu mwimbaji kwa namba za simu zilizopo katika kava hapo chini.


Yelonimo Mwalo audio CD Cover

SIKILIZA WIMBO ULIOBEBA JINA LA ALBAMU "HATUWEZI BILA MUNGU" WA YELONIMO MWALO


 SIKIKILIZA NYIMBO ZAKE KATIKA YOUTUBE KWA KUBOFYA HAPA

Comments