RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EXCLUSIVE: SAMWELI NUNGWANA KUTOKA ARUSHA TANZANIA AMEWEZA KUWEKA NYIMBO ZAKE KATIKA YOUTUBE ILI UKOMBOLEWE.

Samweli Nungwana ni mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Arusha Tanzania. Mungu amempa karama hii ya uimbaji ili aokoe roho za watu kwa njia ya uimbaji wake. Mwimbaji huyu amefanyika baraka kwa walio wengi na hasa waliobahatika kusikia nyimbo zake. Mbali na uimbaji pia mwenyekitiki wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania kanda ya Kaskazini. Hakika ukisikiliza nyimbo zake zina utofauti na uimbaji wa tu wengine, zina upako wa ajabu sana hasa zile alizoimba kama tenzi za rohoni. Mungu anaviumbe vyake hapa duniani vua kumtukuza.


Samweli Nugwana

Tuzidi kuiombea huduma ya mwimbaji huyu ili isonge mbele na watu wengi wakaokoke kwa kupitia uimbaji wa samweli Nungwana. Tutangaze Injili kwa wale ambao bado hawajamjua Mungu. Unaweza kuitangaza injili hii kwa kusapoti kazi za watumishi wa Mungu kwa kununua CD au DVD zao na kuwashirikisha wa ndugu na marafiki wakasikiliza  ujumabe wa  Mungu. Tusiwe watu wa kuwakatisha watumishi wa Mungu katiika huduma yao, kwani tunaamini nao hawawezi kukata tamaa kwani wanajua wanayemtumikia ni Mungu na sio mwanandamu.


Samweli Nugwana

UZUSHI WA RUMAFRICA: Ukimuangalia kwa makini sana mtumishi huyu wa Mungu unaweza ukafikiri ni Askofu Kakobe kwa sura yake...Nimechemsha?????? Basi tupia maoni yako katika rumatz2012@gmail.com

Unaweza kuwasilinana naye kwa simu hii +255767 973 383. Unaweza kupata habari zake zaidi katika blogu inayopenwa na walio wengi www.rumaafrica.blogspot.com.

Nyimbo zimewekwa Youtube  na Rumafrica +255 715 851 523

amweli Nugwana

SIKILIZAMOJA YA WIMBO WAKE


BONYEZA HAPA KUSIKIA NYIMBO ZAKE  YOUTUBE

Comments