RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAINDA NIMEFANYA SANA ANASA, SASA BASI!

STAA wa filamu Bongo aliyeamua kumpokea Yesu, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kipindi cha nyuma alipotangaza kuokoka alikuwa ni kama anamtania Mungu ila sasa ameokoka kikwelikweli.

Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda alisema awali alipofunguka kuwa ameokoka, hakuwa siriasi kwani alikuwa akiendeleza anasa za hapa na pale lakini sasa yeye na Yesu, Yesu na yeye.



Staa wa filamu Bongo Ruth Suka ‘Mainda’akipozi

“Mwanzo nilikuwa kama namtania Mungu, nilisema nimeokoka lakini kimyakimya nilikuwa naendeleza anasa, nimefanya sana anasa lakini sasa basi.

“Huwezi kunikuta sehemu yoyote ya starehe hata siku moja, wala kuniona nimevaa mavazi ya ajabu na hata filamu nikicheza siwezi kuonekana kama mwanzo, nachagua vipande vya kucheza ambavyo haviwezi kunivua wokovu wangu,” alisema Mainda.

Source: Global Publisher

Comments