RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWIGIZAJI WA FILAMU TANZANIA JENIFFER KYAKA (ODAMA) KULA CHAKULA NA YATIMA SIKU YA LEO AMBAYO NI SIKU YA KUZALIWA KWAKE.

Jeniffer Kyaka (Odama) ni mwigizaji wa filamu Tanzania ambaye siku ya leo atakuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa katika ukumbi wa Vijana Kinondoni pamoja na YATIMA.

Akiongea na Rumafrica, alisema ameona ni jambo jema sana kufanya hivyo na hawa ndugu zetu amabo hajajaliwa kuwa na wazazi wao hapa duniani. Yatima hawa ambayo maisha yao yamekuwa magumu sana kutoka na kukosa malezi mazuri na ndugu zao au jamaa zao. Inasikitisha sana kuona yatima anakuwa ni mtu wa kutengwa kutukamwa, kubaguliwa na kufanyiwa vitendo vibaya eti hana wazazi.

Odama alizidi kusema anawashukuru sana walezi wa watoto hao ambao wamewachukua na kuwalea katika vituo vyao, wamekuwa wanatumia muda mwingi wa kuwafariji na kuwatia moyo hawa yatima na pegine kuwapa elimu dunia na elimu ya Kimungu ili waweze kuwa kama watu wengine ambao wana wazazi wao.




Rumafrica inakupongeza sana Odama na kampuni yako ya J-FILM 4 LIFE kwa upendo ulioonyesha kuwakumbuka Yatima










Comments