RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII FLORA PETER ALIVYOHUBIRI SIKU YA JUMATATU 14.07.2014 KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI MBEZI SALASALA DSM

NENO LA MUNGU LINATOKA KATIKA KITABU CHA NYAKATI 2: 20:25-30
Biblia inasema: Nao Yehoshofati na watu wake walipokuja kuchukuwa nyara zao, wakaona kati yao wingi wa mali na mavazi, na johari za thamani walizojivunia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukuwa; nataka na wewe uone wingi wa mali hata kama hauna kitu, imani ni hakika ya mambo yatarajiwayo tena bayana ya yale yasiyoonekana, anza kuona wingi wa mali mbele yako, wingi wa mavazi mazuri mbele yako. Anaza kuona kwanza unafanikiwa ndipo itakuja kutokea kweli, unahitaji cheo, anza kuona unapandishwa cheo.

Nabii Flora Peter ibadani

Biblia inasema: Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka, maana ndipo Bwana alipowabarikia, maana zile Baraka zilikuwa nyingi sana, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu na Yehoshofati mbele yao. Na ili kuirudia Yerusalem kwa furaha, kwa kuwa Bwana amewafurahisha juu ya adui zao; tunakwenda kubarikiwa, nakwambia hii ni wiki yako ya kubarikiwa, yaani watu watakuja mahali hapa, hapa ndipo Yerusalemu, ambapo Yesu anaonekana. Bwana atakwenda kukufurahisha juu ya maadui zako, waliosema njaa itawamaliza, itawamaliza wao hiyo njaa.

Hapo Mungu atakapo kujalia maliwa wa kwanza, ndipo maadui zako watakapo tafuta urafiki kwako. Wakafika Yerusalemu wenye vinanda na vinubi, wakapandia kwenye nyumbani kwa Bwana, kukawa na hofu ya Mungu juu ya falme zote za nchi. Waliposikia ya kuwa Bwana amepigana juu ya adui zao

Comments