RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

DONT MISS THIS.....JISOGEZE WORD ALIVE SINZA MORI...UBURUDIKE NA "NEW DAY" YA DA ANGEL BENARD

Angel Benard unashangaza wengi kwa mambo yako katika ulimwengu wa muziki wa Injili Tanzania. Uimbaji wako ni wa tofauti sana, siwezi fananisha na mwimbaji yeyote Tanzania na nje ya Tanzania, uimbaji wako ni wa tofauti sana. Mbali na uimbaji pia mambo yako ni ya kipekee kuanzia utunzi na vile unafanya ukishika MIC madhabahuni au popote unapoalikwa kwa kazi ya Mungu. Uso wako na kile unachotoa kutoka katika kinywa chako binafsi hunifanya nione mbingu hii hapa. Hakika nabarikiwa sana na uimbaji wako.



Cha kunichosha zaidi ni hivi karibuni ulivyofanya shooting ya DVD yako nchini Kenya, yaani nilibaki mdomo wazi nikifikiria ni jinsi gani Mungu anaweza kumpa mtu maujanja pale anapojibidiisha kwa kazi yake. Nilibahatika kuona ka-clip katika FB nikasema kweli huyu ni Angel ninayemfahamu..!!!.

Juhudi zako Angel zitakuweka mahali fulani ambapo dunia itabaki kusema mwacheni Mungu aitwe Mungu. Tunategemea siku ya uzinduzi wako kutakuwa na vitu vingi vigeni ambavyo hatujazoea kuviona mahali popote.

Nikiangalia historia ya maisha yako ya kimuziki nabaki kuduwaa na kutojiamini kuwa kumbe ukijitenga na ya dunia na kujichimbia mahali fulani, Mungu wetu anaongea na wewe na kutimiza haja ya moyo wako.

Rumafrica inasubiri kwa hamu siku hiyo ili ijipatie maupako kutoka kwako Angel na ninaimani siku hiyo tutatoka na tukiwa tumshiba matumbo yetu. Huyu Mungu ninayemuomba ninamuomba azidi kushika mkono wako na kukuongoza ufike mbali na uweze kutimiza ndoto zako.

Bless be the Name of God

Is me Rulea Sanga

Comments