RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JE UNAJUA DANCER WA AGD ALFA MSANJILA NI MKULIMA MKUBWA TANZANIA NA MWENZAKE FRANCIS MWELA NI KOMEDIANI MKALI WA GOSPO?

Rumafrica katika kamatakamata yake mitaani ilkumbana na dancer maarufu sana Tanzania amyaye  alishiriki video zaidi ya 18 za waimbaji maarufu kwa kucheza, na sasa yuko chini ya Bahati Bukuku. Rumafrica ilifanya naye mahojiano mengi sana mabayo utasiki katika Interview ambayo inaandaliwa kwa sasa. Kilichoishangaza Rumafrica ni kuona kijana mdogo kama huyu ana mawazo makubwa sana na ya kipekee sana ukifananisha na waimbaji wengine wa Injili duniani.

Alfa Msanjila (kulia) aliweza kufunguka na kusema yeye kwa sasa amejikita katika kilimo cha mahindi na alizeti mkoani kwake Dodoma, na pia anafanya kazi ya Mungu kwa kucheza na kuimba. Mungu amemuinua huyu kijana kwa kiasi kikubwa sana katika huduma yake ya kucheza na kuimba.

Kwa sasa wameunda kikundi chao kinachokwenda kwa jina la Africa Gospel Dancers kilicho chini ya mlezi wao Masanja Mkandamizaji wa Ze Komedi.

Mbali na ku-dance pia Mungu amewapa zawadi nyingine ya uimbaji, na sasa wameweza kurekodi nyimbo 4 ambazo zimekalika ma zenye upako wa ajabu. Alfa na wenzake walimshukuru sana Mungu kwa kuwaunganisjha kama vijana sita wanaochapa kazi ya Mungu na kuunda kundi lao la AGD.

Rumafrica ilitupia jicho la pili kwa rafiki yake Alfa ambaye wanafanya naye huduma ya kumtumikia Mungu kwa njia ya dancing ambaye alijitambulisha kwa jina la Fracis Mwela. Kijana huyu ni comedian katika runinga ya ATN hapa bongo. Kazi yake ya kuchekesha aliitambua tangia akiwa mdogo kuwa ana uwezo wa kumfanya mtu acheke kwa kile atakachofanya au kusema. Mungu aliweza kumuunganisha na Alfa na kuunda kundi la AGD

Wakiongea kwa unyeyekevu mkubwa sana waliwaomba wadau kuunga mkono kazi yao hii ambayo wameanza ya kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji wakiwa bado vijana wadogo na wanaopitia kwenye changamoto za maisha. RUMAFRICA INAANDA INTERVIEW YAO NA HUKO UTASIKIA MENGI

Zidi kutembelea www.rumafrica.blogspot upate kujua habari zake na mipango yake

Comments