RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KAMA ULIKOSA KUONA MWIMBAJI WA GOSPO PAUL CLEMENT AKIFANYA KOLABO NA MZEE MZIMA BEN POL..PATA UHONDO NA UTABARIKIWA

Nilichogundua katika hii kolabo ya mwimbaji wa nyimbo za Kidunia na mwimbaji wa nyimbo za Injili ni kwamba kuna hali fulani ya UPENDO kati yao. Si rahisi sana kuona waimbaji wa nyimbo za Injili na za  kidunia wakishirikiana na kuimba wimbo wa kumtukuza Mungu.

Ben Pol
Kitendo walichokifanya hawa jamaa ni kizuri sana na kimetufundisha mengi kati ya washabiki wa pande hizi mbili yaani wale wa gospeli na wale wa kidunia. Kila mtu atakuwa na maoni yake jinsi atakavyoona hii clip.

Rumafrica inawapa big up watumishi wa Mungu, na hasa Paul Clement kuweza kumshawishi rafiki yako Ben Pol kufika katika tamasha lako na kufanya kolabo na wewe. God Bless You..!! Kitu ulichokifanya ni kikubwa sana machoni pa wengi. Kuthubutu kwako kufanya visivyowezekana vimeleta UTUKUFU kwa Mungu.

Paul Clement (kulia)

Ushauri wangu kwako mwimbaji, kama Mungu atakujalia kupata mshiko kidogo jitahidi sana katika kazi yako ya uimbaji uwashirikishe watu wa nyimbo za kijamii kwani ukifanya hivyo utakuwa umewavuta kutangaza kazi ya Mungu kwa wale wadau wa Gopeli na wa nyimbo za Kidunia.

Ben Pol

T9umeona sasa waimbaji wa nyimbo za kidunia kama vile Linex, Alikiba, Barnaba, Beyonce na wengine wengi wameanza kuimba nyimbo za kumsifu Mungu. Rumafrica itakuletea baadhi ya nyimbo ziligongwa na vijana wa Bongo Fleva


Kama  hukufanikiwa kufika kwenye video shooting yake Paul Clement, basi hiki ndicho kilichotokea. Ni ben Paul alipata nafasi ya kuombewa na akaahidi kuwa huwenda siku moja atakuja rudi imba Gospel songs, lakini zaidi ya yote alipata nafasi pia ya kuimba  nyimbo moja na Paaul Clement, itazame sasa.




Comments