RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA RESTORATION BIBLE CHURCH LAJITOA KUOMBEA TAIFA LA TANZANIA KUWA NA AMANI NA UTULIVU

Nchi ya Tanzania ni nchi ya amani na utulivu kwa muda mrefu sana, lakini kanisa la Restoration Bible Church lililoko Kibaha limeona haitoshi, ni lazima kutenga muda maalumu kwaajili ya kulinda hii amani ya nchi tuliyozawadiwa na mwenyezi Mungu kwa kufanya maombezi.

Siku hii itakuwa ya kipekee sana kwa wananchi wa Tanzania watakaoungana na watumishi wa Mungu kuliombea Taifa letu la Tanzania. Mchungaji Deogratias Timbili amejiandaa kufanya kazi ya Mungu na kuhakikisha siku hiyo Mungu kwa njia anazozijua atashuka kwa namna yake kugusa Watanzania wenye nia ya kuguswa siku hiyo.

Katika mkutano huu kutakuwa na mgeni rasmi kutoka Zanzibar, Makamu wa raisi wa Pili wa serikali ya Zanzibar Mh. Baloz Seif Idd. Pia kutakuwa na waimbaji wengi sana kama wanavyoonekana katika tangazo.

Kama Mtanzania ungana na watumishi hawa wa Mungu kuliombea Taifa letu lizidi kuwa na amani na utulivu. Mungu wangu ana akubariki sana

Comments