RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MATUKIO KATIKA PICHA YA UZINDUZI WA ALBAMU YA ATOSHA KISSAVA SIKU YA JUMAPILI -DA R ESA LAA

"KILA MUTU ANASEMA UMWEMA" ndio ulikuwa wimbo wa taifa kwa siku ya Jumapili katika kanisa la PTA Sabasaba kwa Askofu Katunzi. Mwanada Atosha Kissava kutoka Tanzania aliweza kuzindua albamu yake ya "KILA MUTU ANASEMA UMWEMA" kwa mara ya kwanza tangia ameanza kumwimbia Mungu. Tunamshukuru sana Mungu kwa uitikio wa watu siku hiyo. Tunawashukuru sana watu wote mliofika siku hiyo kumuunga mkono mtumishi wa Mungu Atosha Kissava, kwa maana ilikuwa sio kitu cha kawaida kuona watu wengi sana wamekusanyika pamoja kumtukuza Mungu kwa njia ya sifa.

Pia tunashukuru sana waimbaji walioweza kufika katika kumuunga mkono mtumishi wa Mungu Atosha Kissava pamoja na watu wa media ambao walifanyika msaada mkubwa sana kipindi cha kutangaza tamasha hili. Na bila kuwasahau watu walioweza kutoa michango yao kuhakikisha kijana wao anasonga mbele kwa kazi ya Mungu.

Shukrani za dhati kwa Mh. Kapuya kwa kuacha kazi zake na kuweza kuhudhuria tamasha hili na bila kumsahau Askofu Katunzi ambaye aliweza kuruhusu tamasha hili kufanyika katika kanisa lake takatifu. Uongozi mzima wa kanisa la PTA mlifanyika baraka sana kwa upendo wenu na huruma zenu kuhakikisha kazi ya Bwana kupitia mtumishi wa Mungu Atosha Kissava inafanyika kwa asilimia zote.

Tunawaomba sana mfano mlionyesha katika tamasha la Atosha uzidi kutumika hata kwa matamasha ya watu wengine ili tuzidi kutiana moyo na kulitangaza Neno la Mungu kwa njia ya uimbaji. Tunapokuwa wengi tunamtaabisha shetani, kwahiyo tuzoidi kufanya hivyo hata kwa matamasha yajayo. Siku ya jumapili kwa kweli mlimshangaza shetani na kumkimbiza kwa viboko. Tunawapongeza sana watu wa Mungu kwa kazi mliofanya siku ya Jumapili.

Mungu azidi kuwabariki na azidi kuongeza pale ambapo mlitoa kwaajili ya kusapoti kazi ya Mungu isonge mbele. Mungu awabariki sana na tuzidi kuombeana

Wenu katika Bwana
Rulea Sanga
wa 
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS









Comments