RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII FLORA PETER SIKU YA JUMANNE 16.09.2014 ALIFUNDISHA NENO ZURI SANA..TAFADHALI SOMO LITAINUA IMANI YAKO

NENO LA MUNGU LINATOKA KATIKA KITABU CHA NABII ISAYA 14:1-8
Biblia inasema: Bwana amelivunja gongo la wabaya, fimbo ya enzi yao wenyewe wanaotawala; hii ni wiki ya kuponywa na kufunguliwa, Bwana amelivunja gongo la waovu, yaani waovu wote waliokuwa wanakuloga, walioiba nyota yako, walioharibu mafanikio yako, wanaologa afya yako, ndoa yako, kizazi chako, Bwanaamevunja gongo la waovu wote. Amewavunja maadui zako, wachawi wote, waliochukuwa watoto wako.
Biblia inasema: Maana Bwana atamuhurumia Yakobo, atamchagua Israeli tena; Bwana amemuhurumia Yakobo, maana ya Yakobo ni watumishi wake, na ukisikia Yakobo amehurumiwa maana yake ni Mungu amelihurumia Kanisa lake, haijalishi ulitenda dhambi ya namna gani Bwana ameahidi kukuponya na kukufungua.
Biblia inasema : Naye atawaweka katika nchi yao wenyewe, na wageni watajiunga nao,nao wataambatana na nyumba ya Yakobo; tunakwenda kuwekwa katika nchi yetu, walikuhamisha wachawi, wakahamisha mafanikio yako, wakafunga uchumi wako, kazi zako, watoto wako, mke wako, mume wako lakini Bwana amekuhurumia. Bwana atakurudisha katika nchi yako, atakurudishia mafanikio yako, unakwenda kuponywa na kufunguliwa.
Biblia inasema: Na hao mataifa watawatwaa na kuwaleta mahali pao wenyewe, katika nyumba ya Israeli watamiliki; yaani Bwana anakwenda kukufungua, kukutoa ulipotekwa, ataugeuza uteka wako, atakwenda kukutoa kule ulipokuwa umeibiwa nyota yako. Yamkini waliiba nyota yako, mate yako ulikuwa unapiga mswaki, wiki hii ni wiki ya kufunguliwa kwako, Bwana anakwenda kukuponya leo, kwa damu ya Yesu. Tutakwenda kumiliki majumba makubwa, makampuni makubwa, pokea kuponywa, pokea kumili.
Biblia inasema: Na atawafanya kuwa watumishi na wakazi katika nchi ya Bwana, tena itakuwa katika siku ile, ambayo Bwana atakupa raha badala ya huzuni yako. Jinsi alivyokoma mwenye kuonea, jinsi ulivyokoma mji ule wenye jeuri; yaani Bwana anakwenda kukomesha mji ule wenye jeuri, yaani ukisikia mji ni mtu, kuna watu wajeuri kulalia maisha ya watu, Bwana anakwenda kuwavunja maadui zako, na anakwenda kukomesha mji ulio jeuri juu yako. Mateso, magonjwa, laana vinakwenda kukomeshwa, UKIMWI unakwenda kuvunjwa kwa damu ya Yesu Kristo.

Mchungaji Komba (mwalimu wa mambo ya ndoa)
Ufunuo 12:11
Biblia inasema: Nao wakamshinda kwa damu ya mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; tunazo sababu za kumshinda shetani, tunalo neno la ushuhuda, wanaotembea na magongo wanafunguliwa, tunazo shuhuda ambazo tunamshinda shetani kwa damu ya Mwana Kondoo. Vipofu wanaona, vilema wanatembea, Kansa zinaondoka, wasiokuwa na pesa wanapata, wasiozaa wanazaa, waliokufa wanarudi, pokea muujiza wako.

Comments