RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA INATOA POLE KWA KANISA LA SCOAN KWA KUPOTEZA WATU TAKRABANI 50 KWA AJALI YA GHOROFA KUPOROMOKA

Rumafrica inatoa pole kwa kanisa la SCOAN kwa kupatwa na msiba mkubwa sana. Pia tunatoa pole kwa wafiwa waliopotelewa na ndugu na jamaa zao. Tunazidi kuwaombewa wajeruhiwa wa ajali hii ambao wamepata majeraha makubwa. Mungu azidi kumtetea Mtumishi wake TB Joshua kwa kipindi hiki kigumu anachopitia kwa sasa.

Baadhi ya mitandao imeripoti ya kuwa idadi ya watu waliokufa kwenyeghorofa la makao makuu ya Kanisa la SCOAN (Synagogue Church of All Nations) la Nabii TB Joshua wamefikia 50.Jengo hilo la ghorofa tano ambalo ni makao makuu ya kanisa na nyumba ya kulala wageni liliporomoka Jumamosi wakati ujenzi ukiendelea.Hadi kufikia jana Jumapili jumla ya watu 41 walikuwa wameripotiwa kufa, lakini maiti nyingine tisa zimeongezeka leo hii.Inaelezwa kwamba. Uokoaji bado unaendelea na watu wengine 124 walikuwa wameokolewa wakiwa hai hadi kufikia jana Jumapili.

Mmoja wa majeruhi waliookolewa kwenye kanisa hilo akiwa hajitambui.Jengo hilo liko katika eneo la Ikotun magharibi mwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lagos.




Comments