RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ANNA DAT AMSHUKURU MUNGU KUMTOA KATIKA MAISHA YA USELA NA UKOROFI

Anna Dat ni mwimbaji wa nyimbo za Injili ambaye ametokea kumpenda huyu Bwana Yesu Kristo baada ya kuokoa na kuishi maisha mapya yenye furaha na amani. Kabla ya wokovu Anna Dat alikuwa akiishi maisha yasiyompendeza Mungu kabisa, mpaka ilifika kipindi mama yake mzazi alimkana kuwa ni mwanae kutokana na amatendo machavu aliyokuwa akifanya. Maisha yake yalikuwa ni ya ugomvi sana, mtaa mzima walikuwa wanamuogopa kutoka na fujo na kupiga watu.
Kuna kipindi alijiingiza hata kuvuta bangi, amefanya pia kazi za kuuza bar hapa jijini Dar es Salaam. Shetani alimtumia sana Anna Dat na kumharibia sifa kwa jamii iliyomzunguka. Jamii ilimchukulia kama ni mtu aliyechanganyikiwa kutokana na matendo yake mabaya, alijitenga na jamii kabisa, aliishi maisha ya u-gangsta yaani aliishi kama mwanaume kimavazi, kuongea na hata kutembea.

Lakini siku yake na saa yake ilipofika mkono wa Mungu ulimgusa Anna Dat, na kuamua kuokoa. Kitu kilichomsababishia kuokoka ni pale tu alipoamua kurudi kutoka Dar es Salaam na kuelekea kwao Moshi, alipofika huko aliona rafiki zake waliokuwa wakorofi kama yeye wameokoka na wengine wamekuwa wachungaji. Anna Dat alishangazwa sana na ikamsababishia na yeye kuamua kuokoa, na hao wachungaji wakaanza kumfundisha jinsi ya kusali.

Anna Dat mpaka tunaongea sasa amefanikiwa kutoa albamu yake yenye mfumo wa video inayoitwa PINDUA. Jipatie nakala yako sasa madukani

Nisimalize uhondo wa stori hii, unaweza kusikiliza mwenyewe katika mahojiano yaliofanyika na Rumafrica na pia utasikia baadhi ya nyimbo zake alizoimba.
Unaweza kuwasiliana naye kwa simu +255 655369 965

MAHOJIANO


Comments