RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MASANJA MKANDAMIZAJI BAADA YA KUTUA KUTOKA USA ASHIRIKI PARTY NDOGO YA RAFIKI YAKE MC CHAVALA

Mchungaji mtarajiwa Masanja Mkandamizaji baada ya kutua Bongo akitokea Marekani aliamua kuanzisha safari nyingine kuelekea Mbeya katika shughuli ya rafiki yake MC Chavala, ambaye kwa siku ya leo amekabidhiwa mchumba wake.

Kuna jambo ambalo ninajifunza  kupitia mwimbaji na mchungaji mtarajiwa mwana wa Street Gospo  Masanja Mkandamizaji, kwanza anaonyesha ni mtu mmoja anayependa sana kushirikiana na wenzake, ni mtu anayejishusha sana na kuishi maisha ya kawaida ukifananisha na mastaa wa kibongo, ana moyo wa upendo sana, ni mwenye huruma sana, ni mtu anayependa kuona mwingine anafanikiwa. Kumbuka ametoka Marekani na akaona haitakuwa vizuri kuona siku maalumu ya rafiki yake Mc Chavala inapotea pasipo yeye kuwepo, ndio maana akafunga safari mpaka Mbeya. Mungu azidi kumbariki na kumuongezea zaidi ya hivyo alivyonavyo.
 Kulia ni Masanja Mkandamizaji na MC Chavala wakifanya yao kwa utukufu wa Mungu.

 Hiki ni kituko...




Comments