RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA VENERANDA BUGERAHA KUWASHIRIKISHA NA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA SIFA FOUNDATION KATIKA UZINDUZI WA DVD YAKE YA "AMETENDA". SHIRIKI BARAKA HIZI

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Veneranda Bugeraha siku ya Jumapili 30.11.2014 atazindua albamu yake ya AMETENDA katika ukumbi wa Landmark Riverside ulioko Ubungo jijini Dar es Salaam. Tamasha litaanza saa 7:00 mchana na kuendelea, kutakuwa na waimbaji mbalimbali kama vile Mess Jacob, Neema Jekonia, Atosha Kissava, Upendo Nkone, Manesa Sanga, Furaha Isaya, Grace Rwegasha, Ibrahim Sanga na wengine wengi.

Katika tamasha hili kutakuwa na watoto yatima kutoka katika kituo cha kulea watoto yatima cha Sifa Foundation chini ya Sifa John ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Watoto hawa  wataweza kushirikiana na Veneranda katika zoezi kuimba na kucheza siku hiyo, watazungumza matatizo yao wanayokumbana nao katika kituo chao na ile hali ya kutokupata malezi ya mama na baba. Na hiyo yote ni jinsi gani ya kuonyesha upendo kwa watoto hawa ambao wamefiwa na wazazi wao na wamekuwa wakiishi katika maisha magumu, wamekosa faraja, wamekataa tamaa, hawaoni uzuriwa dunia hii, lakini ashukuriwe Mungu kwa kumuinua Sifa John na kuchukua jukumu la kuwalea hata kama wanaishi katika mazingira magumu, Mungu nanazidi kuwatetea.

Veneranda Bugeraha baada ya kukaa chini na kumuomba Mungu juu ya uzinduzi huu aliweza kupata mafunuo ya kuwashirikisha watoto hawa katika uzinduzi wa albamu yake na katika uzinduzi huo  ataweza kutoa zawadi kwa watoto hawa yatima na pia ataweza kuimba nao stejini. Watoto hawa watapata muda wa kuonyesha vipaji vyao ambavyo vimejificha kutokana na kushindwa kuvitumia kutokana na kukosa watu wa kuviona, lakini siku hiyo mtapata kuviona.

Sasa kama ndugu au rafiki unaombwa kuja na kitu chochote kwaajili ya kuwasaidia hawa watoto yatima, waweza kuja na mavazi (kama nguo na viatu vipya au vile ambavyo unaona hutumii), chakula na vinywani.   Pia kutakuwa na maonyesho ya mavazi, watu wataweza kuonyesha ni mavazi gani ya heshima ya kuvaliwa mtu akiwa kanisani, nyumbani, beach, outing, kazini na sehemu mbalimbali.

Unaombwa kufika mahali hapo siku hiyo ili uungane na Veneranda pamoja na watoto yatima. Kwa kuwachangia watoto yatima Mungu atasema nawe katika maisha yako.
Unaweza kuwasiliana naye kwa simu +255 0655 622 250

Kadi na tangazo hii limetengezwa na Rumafrica +255 715 851 523

Comments