RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SAFARI YA MTUMISHI WA MUNGU ASKOFU KAKOBE -4

Makala: Elvan Stambuli
Naendelea kuwaletea mazungumzo kati yangu na Askofu Zakary Kakobe baada ya kuanza kufanya mikutano ya uponyaji na kawaida maeneo mbalimbali.


Kwa siku 256 tu kuanzia Januari 5, 2007 nikianzia Mlali Morogoro na kumalizia Septemba 17, 2007 huko Ngerengere mkoani Morogoro, baadhi ya mikoa nilikuwa nafanya mikutano hadi mitatu kwa siku.
Mwandishi: Ni mikutano mingi sana, yote ilikuwa ya miujiza?

Askofu Kakobe: Hapana. Kati ya siku 256 niliyotumia kuzunguka nchi nzima mikutano ya miujiza ilikuwa 138 na nilikuwa nafanya mikutano mitatu au miwili kwa siku 10 au mikutano miwili kwa siku 53 na mkutano mmoja kwa siku 75. Ukifanya hesabu utakuta nilifanya mikutano 138 kwa siku hizo 256.

Mwandishi: Mikutano hiyo ulikuwa ukiifanya wilayani na mikoani tu?
Askofu Kakobe: Hapana; nilikuwa naifanya hata vijijini kuanzia Kijiji cha Mahurunga, Mtwara, mpakani na Msumbuji ambapo ilikuwa Julai 28, 2007 hadi Kijiji cha Wampembe, wilayani Nkasi kule kando ya Ziwa Tanganyika ambapo nilifika Mei 28, 2007.
Mwandishi: Ni hiyo tu?

Askofu Kakobe: Baada ya hapo nikaenda Bwisya, katika Visiwa vya Ukara Mei 1 2, 2007 hadi Duga Maforoni na Kijiji cha Horohoro, Tanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya hiyo ilikuwa Agosti 16, 2007, safari ingine ikawa kutoka Kijiji cha Kabanga hadi kwenye mpaka wa Tanzania na Burundi, hiyo ilikuwa Mei 16, 2007 hadi Kilindoni na Kisiwani Mafia hiyo ni Juni 28, 2007.

Nikatoka Kijiji cha Njani Marikanda, wilayani Arumeru machi 26, 2007) na nikafika Loliondo Machi 30, 2007, baadaye nikaenda Kijiji cha Mpwayungu wilayani Chamwino, Dodoma Machi 12, 2007 hadi Tunduru ambako nilifika Julai 30, 2007.

Mwandishi: Safari ilikuwa ndefu, baada ya hapo hukuwa na mpango wa kueneza Neno la Mungu kwa mataifa ya nje?Askofu Kakobe: Nilifikiria hilo lakini kabla ya kufanya lolote nilimuomba Mungu ili aweze kuniangazia.


Mungu aliniambia niache, nisifanye hivyo kwa wakati huo maelekezo yake ni kwamba ningefanya hivyo baadaye kwa kushirikiana na Global Body of Christ ambao watanipa nguvu, vifaa na akaniambia atanipa mafundisho ya ziada lakini akanishauri kwamba atanipa nguvu ya kufanya hayo baada ya kunifanya mtoa huduma ya wokovu kimataifa.

Mwandishi: Umewahi kufanya huduma za wokovu na miujiza katika nchi gani?
Askofu Kakobe: Nchi nyingi kwa mfano mwaka 1996 nilikwenda kufanya mikutano India katika Jiji la Pine, mwaka 1999 nikaenda Kandy, Sri Lanka na Nairobi Kenya. Mikutano hiyo ikafungua milango kwa mikutano mingine mingi ya kimataifa. Mwaka 2006 nikaenda Korea ambapo nilishangaza wengi, wakasema hawakuwahi kuona waliyoyaona kutoka kwangu.

Mwandishi: Korea ni mbali sana, ulialikwa na nani?
Askofu Kakobe: Nilialikwa na Korea Revival Mission, ni taasisi kubwa sana kule ipo chini ya Mchungaji Yonggi Cho ambaye ni kiongozi wa Kanisa la Yoido Gospel.

Mwandishi: Hapa Afrika licha ya Nairobi Kenya, wapi kwingine ulikwenda kuhubiri?
Askofu Kakobe: Mwaka 2008 nilienda Burundi, mikutano ilifunguliwa na Mke wa Rais wa Burundi, Denise Nkurunziza. Mikutano ilifanyika kwa siku sita na ilikuwa ikitangazwa live na Redio Vyizigiro (Vizigiro maana yake tumaini) ambayo inasikika nchi yote. Niliwahutubia hata wafungwa katika Gereza Kuu la Mpimba.

Nchi ilitikisika kwa mambo aliyoniwezesha Mungu kuwaonesha watu wa pale, jina la Yesu lilihimidiwa! Mei 9, 2010, nikaenda Lubumbashi (DR Congo) na mikutano hiyo ilifunguliwa na Waziri wa Bajeti, Jean-Baptiste Ntahwa Kuderwa Batumike; mikutano ilifanyika katika Uwanja wa Stade Des Martyrs, na mwaka huohuo nikaenda Lusaka, Zambia mikutano ilifanyika katika Uwanja wa Matero, Yesu akawa gumzo huko.Yote haya nayafanya chini ya taasisi isiyo ya kiserikali ya Bishop Zachary Kakobe International Ministries (BZKIM) ambayo imesajiliwa Marekani na Canada ambako nilifanya mikutano mikubwa ya Injili miaka ya nyuma.

Itaendelea wiki ijayo.

Mwandishi: Kuna waliosema kuwa ulianzisha kanisa huko Marekani na wakasema unahamia huko, je ni kweli?Askofu Kakobe: Kuhama nchi siwezi lakini ni kweli baada ya maombi ya muda mrefu Aprili 16, 2012 nilifungua kanisa Marekani, hii ni nia ileile ya kuokoa mataifa na kuinua jina la Yesu.

Mwandishi: Tunaona watu wakifunga ndoa wanavaa pete lakini katika kanisa lako hamfanyi hivyo, unazungumziaje hilo?Askofu Kakobe: Pete kwenye ndoa siyo agizo la Bwana na ndiyo maana tunaona Mungu mwenyewe akichukizwa na watu waliovaa pete, vikuku na mapambo mengineyo.

Soma maandiko haya ISAYA 3:21, 16-24; Hosea 2:13; Mwanzo35:1-5; Kutoka 33:4-6; Yeremia 4:30; 1 Timotheo 2:9-10; 1Petro 3:3-5. Mapambo ni mavazi ya waabudu miungu, yanahusishwa na ibada ya miungu (mashetani)

Itaendelea wiki ijayo.

Comments