RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WANAKWAYA WA MATENDO EAGT ELERAI SAKINA WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI YA GARI

Kama ni mkazi wa Arusha katika kitongoji cha Sakina, basi bila shaka kanisa la EAGT Elerai Sakina unalifahamu na kwaya hii unaifahamu pia, ambayo juzi ilipatwa na pigo kubwa la kufiwa na wana-kwaya wao watatu kwa ajali ya gari, iliyo tokea majira ya saa saba mchana, ambapo marehemu hao walikuwa wakienda kwenye msiba wa mmoja kati ya washarika wa kanisa lao.

''Aliyefariki ni dereva anaitwa Michael mollel ni muimbaji wa kwaya ya matendo EAGT elerai sakina napia mwingine anaitwa Kivuyo na yeye pia ni muimbaji wa kwaya hyo hyoo na mmama mmoja anaitwa Mrs.Fataeli Mbando na wa mama wawili wamepona'' alisema Papaa Gerald (Church Boy) wakati akituhabarisha juu ya tukio hilo la kusikitisha.

Taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika, ambapo kila mmoja atazikwa siku yake kuanzia leo, ili kuruhusu waumini wa kanisa hilo kushiriki katika kila mazishi, sawa na pendekezo la Mchungaji wa Kanisa hilo, Marko Haule.

Comments