RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ASKOFU BOAZ SOLO KUTOKA IRINGA KUUNGURUMISHA INJILI KATIKA KANISA LA R.G.C TABATA CHANG'OMBE KWA MTUME PETER NYAGA

Kama Askofu Boaz amefunga safari kutoka Iringa mpaka Tabata Dar es Salaama kwaajili yako, kwanini wewe usndwe kutafuta nauli ufike kusikiliza ujumbe alionao kwaajili yako? Kuna kiroho cha shetani kinapuuzia wewe kutoona thamani semina hii iliyoyoandaliwa kwaajili yako. Sasa ili umshinde shetani ni wewe kuamua na kusema sasa naacha kila kitu naenda kwenye semina hii ili nikajifunze jambo ambalo litanisaidia katika maisha haya mafupi ya kuishi hapa dunia.

Najua uko busy sana na kutafuta pesa kwaajili ya wewe kuishi lakini kumbuka Mungu ndio yuko busy sana kuhakikisha kila kiumbe kinapata mahitaji muhimu, na Mungu huyo huyo anayekusaidia anapenda kuona wewe unamtukuza na unakuwepo mahali anapokuwepo ili azungumze na wewe kwa kupitia watumishi wa Mungu walioandaliwa kwaajili yetu.


Kuna Mwinjilisti kutoka Kenya Mwnj. Isack Nyaga ameungana na Askofu Boaz Solo na Mtume Peter Nyaga kufanya kazi ya Mungu ili wewe na mimi siku moja tukakae na malaika katika ile siku ya mwisho huko mbinguni tukiimba na kufura maisha yetu yote yaani milele. Jitahidi ndugu yangu siku hiyo uwepo mahali hapo na Mungu atakutete siku zako za usoni.

Yangu ni hayo
Rulea Sanga

Comments