RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI TANZANIA CHAFANYA SAFARI MKOANI SINGIDA KUFANYA UMISHENI KWA SIKU TATU

SEHEMU YA KWANZA
Picha zimepigwa na Rumafrica +255 715 851523
Habari na Rumafrica
WAIMBAJI NA WACHUNGAJI WAKIWA KATIKA UWANJA WA MLIMANI CITY KUELEKEA SINGIDAI
likuwa siku ya 12.11.2014 mida ya saa 8:00 asubuhi baadhi ya waimbaji wa nyimbo za Injili kama vile Jane Misso, Tumaini Njole, Lilian, John Shabani, Pafii, Stella Joel, Yeronimo Mwalo, Cameraman Danny na Rulea Sanga, Joyce Ombeni, Mama Afande, na wengine wengi walikusanyika katika uwanja wa Mliman City kwaajili ya Safari ya Singida.

Kabla ya safari kuanza waimbaji walifanya MAOMBI ili Mungu azidi kuwalinda katika safari  ya kuelekea Singida kwaajili ya kufanya umisheni kwa siku tatu katika kijiji cha Ushora Kibaya wilaya ya Iramba viwanja vya Kanisa la K.K.K.T Ushora Kibaya. Chama cha Muziki wa Injili Tanzania kikiongozwa na mlezi wao Mh. Martha Mlata waliamua kufanya umisheni katika vijiji kwani watu wengi wamekuwa wakifanya mijini tu, na watu wa kijijini kusahalika.

Mungu aliweza kuwalinda waimbaji hawa katika safari yao na kufika salama kabisa.

Endelea kutembelea blogu huu kujua mengi kuhusiana na safarii hii, vitu gani vilifanyika huko Singida na katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tuamini Njole akielekea kwenye basi tayari kwa safari
Kutoka kushoto ni Pafii, Jane Misso Conductor wa basi, Tumaini Njole, Stella Joel, Edson MWasabwite, John Shabani
 


John Shabani na Edson Mwasabwite
Edson Mwasabwite

Pafii (kushoto) na Edson Mwasabwite


KIPIDII CHA KUIOMBEA SAFARI IWE SALAMA
Jane Misso akiongoza maombezi
Stella Joel akiomba
Tumaini Njole akisali
Pafii katika maombi
Usafiri wa bodaboda maeneo ya Ubungo mataa
Joyce Ombeni na Mama Afande maeneo ya Kimara wakiungana na waimbaji wenzao kwa safari
Edson Mwasabwite akijianda kwenda kununua kitimaji


Comments