RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

EDSON MWASABWITE KUZINDUA DVD YAKE NDANI YA KANISA LA K.K.K.T SINZA

Edson Mwasabwite akiongea na Rumafrica amesema, anamshukuru sana Mungu kwa kumuwezesha kufika hapa alipofika. Ni kwa neema ya Mungu amesema anakwenda kuzindua DVD yake katika kanisa la KKKT Sinza Kumekucha siku ya 07.12.2014 kuanzia saa 7:00 mchana na kuendelea. Hakutakuwa na kiingilio chochote, ni wewe tu kufika na kujumuika pamoja kumshukuru Mungu na kumsifu kwa yale anafanya katika maisha yetu.
Edson Mwasabwite (kulia|) na Danny (kushoto)


Tamasha hili litasindikizwa na Enock Jonas, Beatrice Mwaipaja, Joshua Mlelwa, Atosha Kissava, Christopher Mwahangila, Ibrahim Sanga, Samson Kabata, Madam Ruti na wengine wengi.

Zidi kutmbelea blogu hii kujua mengi kuhusiana na tamasha hili

Comments