RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MH. FREDRICK SUMAYE AKEMEA RUSHWA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU YA VICTOR ARON SIKU YA JUMAPILI 02.11.2014 DCT TABATA SHULE-DAR

UTANGULIZI
Mwandishi: Rumafrica +255 715 851 523
Picha: Rumafrica
Cover la DVD ya Victor limetengezwa na Rumafrica
MC: Bony Magupa (Mtangazaji wa Channel Ten
Mwenyeji: Mch. Swai wa kanisa la DCT Tabata Chang'ombe
Anayezindua:  Victor Aron (Mtangazji wa Praise Power Radio.
Mgeni Rasmi: Waziri Mkuu Mstaafu awamu ta tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Fredrick Sumaye:
Siku ya Tamasha: Novemba, 2, 2014
Kanisa: DCT Tabata Shule, Dar es Salaam Tanzania
................................
Rumafrica kama kawaida yake iliweza kupenya na kuwabamba watumishi wa Mungu wakifanya maombezi makali sana katika ofisi ya mchungaji wa kanisa la DCT Tabata Shule, Mch. Swai. Victor mwana wa Aron akiwa na waimbaji wenzake walimtanguliza kwanza Mungu kabla hawajapanda madhabahuni kwaajili ya uzinduzi wa aalbamu yake ya 2x 2. Maombi hayo yalikuwa ya muda mrefu sana, na watu walionekana wakimnyenyekea Mungu ili awalinde na adui shetani asije akaharibu kile walichokipanga kwa utukufu Wake na pia waliweza kumshukuru Mungu kwa kuwalinda tangia walipoanza mazoezi ya maandalizi na sasa wamefikia tamati.

Tamasha hili lilifanyika katika kanisa la DCT Tabata Shule siku ya JUmapili 2/11/2014 na mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mh. Fredrick Sumaye. Tuone baadhi ya picha.

BAADHI YA WAIMBAJI WALIOMBA SIKU HII

Kanisa la DCT Tabata Shule
 Mch. Swai wa kanisa la DCT Tabata Shule

MC Bony Magupa wa Channel Ten





 Mdogo wake na Victor Aron
 Neema Jekonia

 Ibrahim Sanga na crew yake


Madam Ruti wa Jana imepita



 Victora Aron wa pili kutoka kulia akiwa na waimbaji wenzake wakifanya maombi






MH. SUMAYE AKIINGIA OFISI KWA MCH. SWAI WA KANISA HILI LA DCT

Mh. Sumaye akielekea ofisini kwa Mch. Swai
Mh. Fredrick Sumaye  akiweka saini katika kitabu cha wageni ofisini kwa Mch. Swai

KIPINDI CHA MH. SUMAYE KUWASALIMIA WAUMINI WALIOFIKA KATIKA TAMASHA.


KIPINDI CHA VICTOR ARON KUMKABIDHI MGENI RASMI MH. FEDRICK SUMAYE RISALA

Victora alimshukuru sana kwa upendo wake na hurumazake za kumuwezesha kufikia hapo alipofikia. Alimshukuru sana Mh. Sumaye kwa kukubali kufika katika tamasha lake. Victor alisema hadi siku ya Jumanne wiki wa mwishi ya tamasha alikuwa hajampata mgeni rasmi wakati tamasha lake linatakiwa kufanyika siku hii ya Jumapili. Mungu aliweza kuzungumza na Mh. Sumaye, kwa maana alipopeleka ombi lake naye alikubali kufika.
Victor Aron akimshukuru Mungu kwa kumuwezesha mgeni rasmi kutii kufika katika tamasha lake.
 Victor Aron akimkabidhi mgeni rasmi risala
 Victor Aron akimsalimia Mzee wa kanisa mzee Shoo
 Kushoto ni Mchungaji wa kanisa la DCT Tabata Shule, Mch. Swai

KIPINDI CHA MCH. SWAI WA KANISA HILI LA DCT KUMKARIBISHA MGENI RASMI MADHABAHUNI.

Mch. Swai kabla hajamleta mgeni rasmi alimshukuru sana Mungu kwa kuweza kupata kibali cha kuwa na ugeni mzito katika kanisa analoliongoza la DCT. Alimshukuru sana Mh. Sumaye kwa unyenyekevu wake kama kiongozi mkubwa katika taifa la Tanzania na aliyewahi kushika nyadhifa za juu kama vile Waziri Mkuu ta Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweza kuacha kazi zake zote na kufika kuungana na Victor Aron.
Mch. Swai wa kanisa hili la DCT Tabata Shule
Mch. Swai na Victor Aron
Mch. Swai na Victor Aron

SALAMU ZA MH. SUMAYE KWA WATANZANIA WALIOFIKA KATIKA TAMASHA.
Mh. Fredrick Sumaye alianza na kuwasalimu waumini waliohudhuria tamasha hilo baada ya kukaribishwa na Mch. Swai madhabahuni. Alimshukuru Mungu kwa kupata mwaliko huu wa kushiriki katika tamasha la Victor Mwana wa Aron.

MH. SUMAYE AKIMPONGEZA VICTOR ARON KWA KUMUALIKA KATIKA TAMASHA LAKE
Alimpongeza Victor Aron na vijana wote wenye kipaji na wako tayari kumtumikia Mungu. Mh. Sumaye aliwashukuru waandaji wa tamasha hili la kipekee Tanzania. Alisema kazi ya kueneza kazi ya Mungu si kazi rahisi, kwani katika Biblia tunasoma kuwa Manabii wa zamani walikuwa na maisha magumu sana, kwasababu mara nyingi unawaambia watu waache yale wanayoyafurahia na kufanya yale yanayompendeza Mungu lakini watu hawafuatilii hayo.  Lakini kwa njia ya uimbaji watu wanakuwa makini sana kwasababu wanaburudika na kupata ujumbe

MH. SUMAYE AKIONGELEA JUU YA VIONGOZI BORA
Akiongea kwa uchungu Mh. Sumaye kuhusiana na RUSHWA Tanzania, alisema , jinsi Taifa linavyomjua Mungu ndivyo Taifa hilo linapata baraka mbele za Mungu. Ili maendeleo yaende vizuri, yawe ya maendeleo au mambo mengine mazuri lazima Mungu awepo.

Kama tunavyokumbuka mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, na kipindi cha uchaguzi amani inaweza kutoweka, watu wanaweza wakakwaruzana. Katika nchi yetu kuna vyama vingi vya kisiasa kama vile CHADEMA, CUF, CCM n.k, na kutokana na vyama hivyo unaweza kuona upendo unapotea kutoakana na kuona eti mwingine yuko chama hiki na mwingine kile. Kwahiyo katika kipindi hiki cha uchaguzi vyama vyetu visikubali kufarakana na viongozi wa vyama hivi wasiweze kufarakanisha wafuasi wao wakaanza kugombana wenyewe kwa wenyewe. Tunawaomba sana kusiwe na mchezo wa kuchezea hii amani tuliyonayo sasa, Watanzania lazima tusimame imara kukataa uvunjifu wa amani Tanzania. Ukiona Chama chochote kimebeba nondo au jiwe, basi tambua hawa hawafai kabisa katika jamii yetu.
Aliendelea kusema, vyombo vya dola na serikali nzima lazima isimamie amani wakati wa uchaguzi na kuhakikisha haki inatendeka. Kama haki haikutendeka kuna watu watasema Baba hapa tunaona unatukwaza.
Jambo la pili aliloweza kuzungumzia ni namna ya kupata viongozi bora. Uongozi ni jambo lililotoka kutoka kwa Mungu kwa nidhamu sana. Musa alipowaoongoza Waisrael, akaona mzigo ni mkubwa, baba mkwe wake akamwambia, mkwe wangu hii hali itakushinda.

Watanzania wa sasa ukiwauliza kiongozi bora ni yupi, nao watasema ni yule mwenye hela. Ndugu Watanzania hivyo ndivyo tunavyoharibu nchi.

MH. SUMAYE AKIKEMEA RUSHWA
RUSHWA, tangu lini uongozi ukasifiwa kwasababu ya kuhongwa. Rushwa ni dhambi na kila mmoja anajua hilo, sasa kama ni dhambi, kwanini wewe unapokea rushwa. Utaona mtu anaomba  kuwa mwenyekiti wa mtaa au mbunge wa jimbo, utasikia anasema nitagawa khanga au fedha, huu si udhalimu, mtu huyu utaona kipindi cha nyuma ukimuomba fedha kwaajili ya wanafunzi waliofukuzwa shule anasema sina fedha. Leo hii uchaguzi umekaribia utakuta viongozi wanakuja na mabahasha yenye fedha, hii tunasema ni jeuri na haikubaliki kabisa.

Viongozi hawa wakishachaguliwa kwa rushwa utaona wanaanza kuwakana waliowachagua wanapokuwa na shida, ukiwauliza wanasema, mimi nilikununua kipindi cha uchaguzi na nikakupa fedha, leo hii unataka nikusaidie mambo yako, mimi yananihusu nini? Sina msaada wa kukusaidia... Watanzania hatuoni hilo, tumekuwa tukifanya haya bila ya kuangali kuwa huyu mtu tunayemchagua atatufikisha wapi. Sasa basi wewe unayepokea hiyo rushwa unatakiwa kutambua kuwa umetenda dhambi.

Dhambi kubwa ambayo haifutiki ni ile ya kumuweka mtu aliyekupa rushwa madarakani, sasa kama unataka kutenda dhambi ambayo unaona jumapili utatubu ni kuhakikisha unapokea rushwa lakini humchagui. Ukipokea Rushwa na ukamuweka madarakani akawa kiongozi, dhambi hiyo haifutiki, kwa sababu huyo yuko pale na anatesa roho za watu, anatesa maskini...sasa wewe utasamehewaje wakati watu wanateseka kutokana na kiongozi uliyemchagua kwa rushwa.
Kwahiyo ninachowaomba Watanzania ni kuwachagua viongozi waadilifu na ambao huwatilii mashaka

Mwalimu Nyerere alituambia mtoa rushwa na yeye ni mla rushwa, kwasababu ni lazima niwadhulumu watu ili niwape pesa kwa lengo fulani. Ninawaomba Watanzania tuwachague viongozi watakaotoa baraka katika nchi hii,  viongozi watakapiga magoti mbele za Mungu na Mungu atawasikia na sio viongozi wabovu ambao hata wakipiga magoti na suruali zao kuchanika, na magoti yao kuchubuka lakini Mungu hawasikii. Wachungaji mnatakiwa kwanza kukemea Watanzania waache mabaya na baadae kuwaombea na sio kuwaombea kwanza huku hamkemei mabaya kwa kuwaogopa watapungua katika makanisa yenu.

Lazima tuchague viongozi wenye hofu ya Mungu, na tendo la kupokea rushwa katika nchi ya Tanzania ni jambo la kudhalilisha na linaweza kuangamiza nchi yetu. Watu wengi hawapendi sana ninapoongelea suala la rushwa na wanajitahidi sana kunikwamisha nisizungumzie suala hili, lakini mimi ninasema, "KUZUNGUMZIA RUSHWA SIACHI"

MH. SUMAYE AKIELEZEA MUALIKO WAKE WA KUFIKA KATIKA KUMUUNGA MKONO VICTOR ARON.
Jamani kijana wetu ametualika hapa ili tuweze kuzindua albamu yake, na kuzindua albamu hiyo atataka albamu hiyo iuzwe ili aweze kuendelea na hii kazi ya Mungu, sasa kama wewe utashindwa kununua DVD yake ataendeleaje, kwahiyo unaombwa sana kunua DVD yake ili apate fedha kwaajili ya kazi ya Mungu. Ningependa kuona kila Mtanzania anakuwa na hii DVD ya Victor Aron nyumbani mwake.

MWISHO
Mh. Sumaye aliweza kumaliza kwa kuwapongeza waumini wote waliofika katika tamasha hili.

KIPINDI CHA KUZINDUA ALBAMU YA 2 x 2 (KANUNI)

Mh. Fredrick Sumaye akionysha DVD iliyotengezwa na Rumafrica baada ya kukata utepe

KIPINDI CHA KUNADI DVD YA VICTOR ARON
Mke wa Victor Aron (kulia)
Mh. Sumaye akimkabidhi Mch. Swai DVD aliyonunua kwa Milioni 1
Mh. Sumaye akimkabidhi dada huyu mlemavu wa mguu DVD aliyonunua kwa 1,700,000














Mtangazaji Erick Brighton (kulia)

Comments