RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TAMASHA LA SIKU TATU LA CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI TANZANIA LAFANA MKOANI SINGIDA LIKIONGOZWA NA MLEZI WA CHAMA HICHO MH. MARTHA MLATA

Chama cha Muziki wa Injili Tanzania kikiongozwa na mlezi wa Chama hicho Mh. Martha Mlata Mbunge CCM Viti Maalum mkoa wa Singida, kilifanya ziara mkoani Singida, wilaya ya Iramba, jimbo la teule la Ushora,  tarafa ya Ndago-Kibaya  katika viwanja vya  kanisa la K.K.K.T.

 Madhumuni ya kufanya ziara hiyo ilikuwa ni kufanya umisheni kwa muda wa siku tatu, kufundisha Neno la Mungu , kuwaombea wale wenye uhitaji, kuliombea Taifa la Tanzania amani na utulivu na pia kufanya tamasha kubwa la waimbaji kutoka Dar es Salaam, Arusha na kwaya mbalimbali kutoka Singida.

Katika tamasha hilo kulikuwa na mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha, Mh. Mwigulu Nchemba ambaye aliwakilishwa na Mh. Margreth Sitta. Tunamshukuru sana Mungu kumsaidia mgeni huyu kuweza kuchangia ujenzi wa Kanisa la jimbo teule la ushirika wa Ushora K.K.K.T tarafa ya Ndago Kibaya.

Baadhi  ya waimbaji walioshiriki katika tamasha hili ni Jane Misso, Lilian, Ann Annie, Stella Joel, Joyce  Ombeni, Beatrice Mwaipaja, John Shaban, Cosmos Chidumule, Pafii, Yeronimo Mwalo,Edson Mwasabwite, Madam Ruti, Enock Jonas, Ibrahim Sanga na mdogo wake, Tumaini Njole, Bupe Kingu, Kwaya kutoka Singida.

Mbali na waimbaji pia kulikwa na wachungaji kama vile Mch. Vaileth kutoka Arusha,  Mch. Bupe Kingu kutoka Dar es Salaam na wachungaji wenyeji wa kanisa la K.K.K.T Ushora Kibaya. Kwa kupitiaa maombezi yaliyofanyika na wachungaji hawa, watu wengi waliponywa na wengine kuokolewa kutoka katika vifungo vya  shetani. Baadhi ya watu walishuhudia matendo makuu ya Mungu kwa kupitia huduma ya waimbaji na wachungaji. Wachungaji waliweza kufanya umisheni kwa kuongea na mtu mmoja mmoja na kmuombea.

Wanakijiji wakiongea na waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo kama vile Rumafrica na Star TV walisema, mara yao ya kwanza kufanyika jambo hilo tangia kijiji kimeanzishwa, hakuna mchungaji yeyote au kikundi chochote kile kilichoweza kufanya jambo hili. Wakiongea kwa furaha na kumpongeza Mh. Martha Mlata kama mbunge wao wa mkoa wa Singida walisema Mungu azidi kumlinda na kumuongezea miaka mingi na heri duniani kutokana na moyo wake wa huruma, upendo na jinsi anavyokisaidia kijiji hicho kwa mambo mengi kama voile kusaidia mahitaji ya wanafunzi na walimu, ujenzi wa makanisa na barabara, kuwasikiliza wenye uhitaji na kuwasaidia, kuwafundisha kujituma na kufanya kazi, kulea familia zao ili baadae zifanyike kuwa msaada katika Taifa la Tanzania.

Katika ziara hiyo pia kulikuwa na upandaji wa miti, wachungaji, waimbaji, waandishi wa habari  waliweza kupanda miti kwaajili ya utunzaji mazingira. Pia kulikuwa waliweza kuliombea taifa la Tanzania mani na utulivu.

Baada tamasha kumalizika mkoani Singida safari ilielekea Bungeni Dodoma kuungana na wabunge katika kikao cha Bunge kinachoendelea hapo Bungeni. Waimbaji waliweza kuingia Bungeni kwa mara ya kwanza na kuweza kujifunza mengi kuhusu Bunge la Tanzania. Waimbaji waliweza kupiga picha na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Nyarando, Mbunge wa CCM Viti Maalum – Singida Mh. Martha Mlata, Mbunge wa Viti Maalum CCM – Mbeya Mh. Marry Mwanjelwa, Mh. Magreth Sitta na wengine wengi.

Ziara ilihitimishwa kwa kupata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mh. Nyarando ndani ya Dodoma Hotel. Mh. Nyarando aliweza kuwashukuru waimbaji kwa ushiriakiano wao na jinsi walivyoweza kujitolea  kufika vijijini kufanya kazi ya Mungu. Pia aliweza kuwaahidi waimbaji kutembelea Ngorongoro Crater ili kujifunza mambo mengi, kutangaza vivutio vya utalii.

Mh. Martha mlata naue aliweza kumshukuru Mungu kwa kuweza kufanikisha zoezi zima la umisheni mkoani kwake.

MATUKIO KATIKA PICHA

Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Singida Mh. Martha Mlata akimkaribisha mgeni rasmi
 Muwakilishi wa mgeni rasmi, Mh. Margreth Sitta akiwashukuru waimbaji na wachungaji


Mdau wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania
Tumaini Njole akifanya yake siku hiyo kwa utukufu wa Mungu

 Kutoka kulia ni Lilian, Rulea Sanga, Mc. Vaileth, Mh. Martha Mlata, Mch. Bupe Kingu, Mh. Magreth Sitta
 Ann Annie akimtukuza Mungu. Kushoto ni Katibu Mwenezi wa CHAMUITA, Stella Joel

Mwimbaji  Beatrice Mwaipaja
 Mwimbaji Edson Mwasabwite
 Mwenyeji wa kijiji cha Ushora ambaye ni mlemavu wa kuongea (bubu) akimwimbia Mungu hata kama ni bubu
Kushoto ni mwimbaji Enock Jonas akiwa na Mh. Martha Mlata siku ya pili ya umisheni

 Ibrahim Sanga akimtukuza Mungu kwa uimbaji
 Mh. Magreth Sitta (kushoto) na Mh.Martha Mlata
 Mwimbaji John Shaban akimwimbia Mungu wetu wa mbinguni
Madam Ruti wa jana imepita akifanya kazi ya Mungu kwa uimbaji

 EnockJonas akiwa amebebwa na wanakijiji wakati akiimba


Pafii

 Cosmos Chidumle

 Cosmos Chidumle siku ya pili ya umisheni
Yeronimo Mwalo

 Picha ya pamoja ya waimbaji na wachungaji

Mwinjilisti kutoka Arusha akihubiri

 Mchungaji Vaileth kutoka Arusha akihubiri
 Mwimbaji Edson Mwasabwite akiwaombea wanakijiji wakati maombezi yakiendelea madhabahuni na Mch. Vaileth kutoka Arusha
Mwimbaji Enock Jonas wa Zungukazunguka  akiwaombea wanakijiji wakati maombezi yakiendelea madhabahuni na Mch. Bupe Kingu kutoka Dar es Salaam
 Mch. Bupe Kingu kutoka Dar es Salaam akifanya maombezi
 Mwimbaji John Shabani akiwaombea wanakijiji


BAADH YA WANA USHORA WALIOSHUHUDIA MATENDO MAKUU YA MUNGU
 Kulia ni Mch. Vaileth (Arusha) na kushoto ni Mch. Bupe Kingu (DSM) wakisikiliza shuhuda



KIPINDI CHA KUFANYA UMISHENI
Mwimbaji Joyce Ombeni (Dar es Salaam) akimsikiliza mkazi wa Ushora Kibaya na baadae kumuombea ndani ya kanisa la kijiji hicho la K.K.K.T
 Mch. Vaileth (arusha) akimsikiliza mkazi wa Ushora Kibaya na baadae kumuombea ndani ya kanisa la kijiji hicho la K.K.K.T
 Mwimbaji Cosmos Chidumle (DSM) akimsikiliza mkazi wa Ushora Kibaya na baadae kumuombea ndani ya kanisa la kijiji hicho la K.K.K.T
Mwinjilisti (Arusha) akimsikiliza mkazi wa Ushora Kibaya na baadae kumuombea ndani ya kanisa la kijiji hicho la K.K.K.T

KIPINDI CHA UPANDAJI MITI-KUTUNZA MAZINGIRA
 Jane Miso akiongea jambo na wanafunzi wakati kushoto ni Mh. Martha Mlata akiwa na furaha kwa ugeni uliomtembelea kijijini kwake
 Waimbaji, wanakijiji, wachungaji na maaskofu wakifanya maombezi na kugawana miti tayari kwa zoezi la upandaji
 Mh. Martha Mlata akiongoza msafara kuelekea katika shamba la miti
Waimbaji wakielekea kupanda miti. Kutoka kushoto ni Mch. Bupe Kingu, Enock Jonas. John Shaban, Madam Ruti, Tumaini Njole, Ibrahim Sanga, Beatrice Mwaipaja. Edson Mwasabwite, Ann Annie

 Msafara wa kwenda kupanda miti ulivyofana
 Mh. Martha Mlata akipanda mti
 Mwimbaji Cosmos Chidumle akipanda mti
 Stella Joel akipanda mti

Kutoka kulia ni Jane Misso na kushoto ni John Shabani
Mwimbaji Ann Annie kushoto akinawa maji baada ya zoezi la kupanda miti, pembeni ni Tumaini Njole
Wa pili kutoka kushoto ni Edson Mwasabwite
Wa tatu kutoka kulia ni Mch. Vaileth kutoka Arusha

KIPINDI CHA KULIOMBEA TAIFA LA TANZANIA AMANI NA UTULIVU
Waimbaji, wanafunzi, wachungaji na wenyeji wa Ushora Kibaya wakiliombea Taifa la Tanzania Amani na utulivu, baada ya hapo uliimbwa wimbo wa Taifa




KIPINDI CHA KUANGAI SINEMA
Wazee, vijana, watoto walikusanyika pamoja kuangali sinema kuhusu maisha ya Yesu na Samson na Delila

MH. NYARANDO NA MH. MARTHA MLATA WAKIONGEA NA WAIMBAJI KATIKA HOTELI YA DODOMA
Kulia ni Mh. Nyarando na Mh. Martha Mlata
Kutoka kulia ni Mzee Cosmos Chidumle, John Shabani, Edson Mwasabwite, Mh. Nyarando, Danny, Lilian, Pafii, Joyce Ombeni, Madam Ruti, Yeronimo Mwalo, Ann Annie, Jane Misso, Tumaini Njole, Stella Joel na Mh. Martha Mlata

Comments