RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

TUNABISHA HODIIII...WAKAZI WA SINGIDA..MTUPOKEE JAMANI TUMETOKA MBALI

Ki ukweli tunamekaribia kufika kwenu wakazi wa Singida, tunawaomba mtupokee tumebeba mizigo mizito sana kutoka kwa Bwana kama zawadi kwenu. Mtusaidie kuibeba na kutuonyesha mahali tupumzike..Hakika Mungu kwa kupitia watumishi wake tumekuja kuleta kile tulichoambiwa na Mungu kwaajili yenu. Tunashukuru kama mmetusikia jamani. Tumeacha mikoa yote tumeamua kuja Singida, tumeacha familia tumeona ni bora kuwasalimia watu wa Mungu wa mkoa huu wenye baraka za Mungu. Tutakuwa na UMISHENI wilaya ya Iramba na siku ya Jumapili tutakuwa na tamasha kubwa sana Singida mjini..mtupokee jamani....

Comments