RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

VENERANDA BUGERAHA KUZINDUA DVD YAKE YA "AMETENDA" NDANI YA HOTEL YA LANDMARK - RIVERSIDE UBUNGO. FASHION SHOW ITABAMBA MIYO YA WENGI SIKU HIYO

Ilikuwa mwezi na sasa ni siku..Dada yetu Veneranda anazindua DVD yake ya ametenda ndani ya ukumbi tulivu wa Landmark Hotel ulioko Riverside Ubungo mkabala na kibao cha Mzee wa Upako Antony Lusekelo.

Veneranda Bugeraha akiwa amependeza

Katika tamasha hili kutakuwa na Fashion Show na wafuatao wataonyesha mavazi ya mtu aliyeokoka anapaswa kuvaa mbele ya jamii na mbele za Mungu, nao ni  Beatrice Mwaipaja, Upendo Nkone, Smart Boy, Mess Chengula na waimbaji mbalimbali wataonyesha mavazi katika FASHION Show hiyo.

Tamasha litakuwa siku ya Jumapili 30.11.2014 na litaanza saa 7:00 mchana na kuendelea, kiingilio kwa watoto ni Tshs. 2000. Wakubwa ni Tshs. 5000 tu.

Waimbaji unaowafahamu wewe watakuwepo mahali hapo kama vile Yohana Kubanda, Stella Joel. Atosha Kissava, Mess Chengula, Madam Ruti, Ibrahim Sanga, Joshua Mlelwa, Grace Rwegasha, AGD, Neema Jekonia, Yeronimo Mwalo, Upendo Nkone na wengine wengine kama utakavyowaona katika tangazo hapo chini. Usikose mtu wangu katika kazi ya Bwana.


Comments