MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

WANAMUZIKI WA INJILI TANZANIA WALIVYOPOKELEWA KATIKA KIJIJI CHA USHORA - KIBAYA WILAYA IRAMBA MKOA WA SINGIDA KATIA ZIARA YA UMISHENI

SEHEMU YA NNE

Mwandishi na mpiga picha: Rumafrica
Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania kilifanya ziara katika kijiji cha Ushora Kibaya mkoani Singida kwa lengo la kufanya umisheni. Chama hiki kikiongozwa na mlezi wao Mh. Martha Mlata, Mbunge wa  viti maalumu (CCM) mkoani Singida. Waimbaji wa chama hicho waliwasiri na kupokelewa vizuri na wananchi wa kijiji hicho. Safari kutoka Dar es Salaam ilianza mida ya saa 3 asubuhi na kuwasili mida ya saa 6 usiku.

Mh. Martha Mlata

Baada ya kufika katika kijiji hicho wageni na wenyeji waliweza kumshukuru Mungu na pia waliweza kutambulishana. Mh. Martha Mlata alimshukuru sana Mungu kwa kupata ugeni mkubwa sana katika kijiji chake, akiamini ya kuwa watu wengi wataenda kuokolewa katika mateso waliyonayo. Katibu Mwenezi wa CHAMUITA Stella Joel naye aliwashukuru wanakijiji kwa na uvumilivu wa kuwasubiria mpaka usiku, na pia alimshukuru Mungu kwa niaba ya waimbaji wenzake kwa kuwasafirisha salama. Zoezi la kutambulishana lilipomalizika watu waliweza kuonyeshwa mahali pa kulala.

Dhumuni la ziara hii ni kueneza Injili vijijini na kuwaleta watu kwa Yesu, kuliombea Taifa Amani na utulivu, utunzaji mazingira kwa kupanda miti, kuwaombea wenye uhitaji, kuwaburudisha waimbaji kwa njia ya uimbaji, kuwasidia wanakijiji kimwili na kiroho.

Mh. Matha Mlata
Chama cha Muziki wa Injili Tanzania kiliweza kutoa huduma kwa muda wa siku tatu. Katika umisheni huu kulikuwa na tamasha kubwa sana ambalo liliongozwa na waimbaji maarufu wanaofahamika hapa kwetu Tanzania kama vile Edson Mwasabwite, Lilian, Joyce Ombeni, Paffii, Stella Joel, Cosmos Chidumle, Jane Misso, Beatrice Mwaipaja, Ibrahim Sanga na mdogo wake, Enock Jonas, Madam Ruti, John Shabani, Ann Annie, Mh. Martha Mlata, Yeronimo Mwalo na wengine wengi. Pia kulikuwa na wachungaji kama Mch. Bupe Kingu, Mch. Vaileth kutoka Arusha na wainjilisti na Maaskofu wa wilaya ya Iramba

Mbali na tamasha kulikuwa na mahubiri kutoka kwa wachungaji na maaskofu, mida ya jioni wanakijiji waliweza kuangalia sinema zenye mafunzo ya Kimungu kama vile kujua maisha ya Yesu Kristo, maisha ya Samson na Delilah na mambo mengi.

Endelea kutembelea blogu hii kwani utaweza kujua mengi kuhusiana na ziara hii ya waimbaji Tanzania. Mambo gani yalifanyika katika kijiji cha Ushora Kibaya? Utajua historia ya kijiji hicho.Utasikia wazo na Mh. Martjha Mlata juu ya kuanzishwa kwa chama hiki cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA), utajua mwanzilishi wa kijiji cha Ushora Kibaya na mambo mengi.

Rumafrica ilihusika katika kupiga hizi picha na kuandaa hii habari ilua kilichoajili Ushora Kibaya.
.Waimbaji wakishuka kwenye busi baada ya kufika
Mwimbaji Pafii akisalimiana na wanakijiji
 Edson Mwasabwite akisalimiana na Wana-Ushora Kibaya baada ya kuwasiri


 Mh. Martha Mlata akiwa akimwelekeza Jane Miso mahali pa kukaa baada ya kushuka kwenye basi

KIPINDI CHA SIFA NA KUABUDU KILIFIKA

 Jane Miso akijitambulisha
 Mwenye nguo nyeusi ni Jane Miso akicheka na Mh. Martha Mlata
 Wachungaji wa kanisa la K.K.K.T Ushora Kibaya wakiongea machache na wageni kutooka DSM ana Arusha
 Katibu Mwenezi wa CHAMUITA akiwashukuru wanakijiji kwa uvumilivu wao na akiwatambulisha wageni alioongozana nao

Mch. Vailteth kutoka Arusha

Mh. Martha Mlata akiwakaribisha wageni wake katika viwanja vya kanisa la KKKT Ushora Kibaya
Camera man Danny (kulia) akifanya yake
0