HATIMAYE TUMAINI NJOLE KUZINDUA ALBAM YAKE MPYA YA MUNGU ANAWEZA


Tumaini Njole ambaye ni gumzo hapa Tanzania kwa uimbaji wake na kucheza kwake. Hakika ukiomuona huwezi kuamini vitu anavyofanya anapokuwa jukwaani. Mungu amempa kitu cha tofauti huyu dada ukifananisha na watu wengine. Tunajua ya kwamba Mungu wetu wa mbinguni amegawa vipaji kwa kila mtu, lakini hiki cha Tumaini Njole ni cha kipekee sana. Tumeona watu wengi wanafunguliwa kutoka na uimbaji wake. Mbali na uimbaji pia ni mhubiri mzuri sana, watu waliobahatika kusoikia mahabiri yake wataamini haya nayosema kwako. Tuzidi kumuombea mtumishi wa Mungu ili azidi kusonga mbele kwa kazi ya Mungu.

Tumaini Njole

Tunamshukuru sana Mungu wetu wa mbinguni kwa kumuumba mtumishi wake Tumaini Njole ambaye amefanyika chachu kwa walio wengi. Watanzani tunajivunia sana kuwa na mwimbaji shujaa na anayepigana kuhakikisha Injili ya Yesus Kristo inasonga mele. Juhudi zake za kumtafuta Mungu zinamfanya aonekane kama nyota ing'aayo.

Siku ya Jumapili hii ndani ya kanisa la K.K.K.T Sinza Kumekucha atakuwa anazindua ile albamu yake mototo toleo la pili baada ya kutoa ya SEMA NA YESU. Watanzania mnakaribishwa sana katika uzinduzi huu wa kipekee sana. Kutakuwa na waimbaji zaidi 30 watakavamia madhabahu na kusambaratisha kazi za shetani.
0