RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SHUHUDA MBALIMBALI KUTOKA KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI KWA NABII FLORA PETER

NENO LA MUNGU LINATOKA KATIKA INJILI YA MTAKATIFU MARKO 5:35-42
Biblia inasema: Hata alipokuwa katika kunena, wakaja watu kutoka kwa Yule mkuu wa Sinagogi wakisema, binti yako amekwisha kufa kwa nini kuzidi kumsumbua mwalimu? Lakini Yesu alipolisikia lile neno likinenwa; yamkini hata wewe unaweza kujipenyeza ukafika kwa mtumishi wa Mungu, kuna watu wamekukatisha tamaa, wanakwambia tatizo ulilonalo, tazama kisukari umekwisha kuoza hauweza kupona, mwambie wewe ni mwanadamu tu, inapofikia mwisho wa mwanadamu ndipo mwanzo wa Mungu kutenda. Watu wengi wamekuwa wakikatishwa tamaa, wakivunjwa moyo, usikubali kukatishwa tamaa wewe songa mbele tu.


Biblia inasema: Lakini Yesu aliposikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa Sinagogi, usiogope amini tu, wala hakumruhusu mtu afuatane naye ila Petro na Yohana na Yakobo, wakafika nyumbani kwa Yule mkuu wa Sinagogi. Akaona ghasia na watu wakilia wakifanya maombolezo makubwa, alipokwisha kuingia, akawaambia, mbona mnafanya ghasia na kulia; yamkini hata wewe watu wamekudharau, wanasema tumwone kama atafika popote, hakika nakwambia unakwenda kufika popote, utaona maisha yako yakibadilika, utaona mipango yako inafunguka.

Biblia inasema: Yesu akawaambia kijana hakufa bali amelala tu, wakamcheka sana, naye alipokwisha kuwatoa nje wote; yamkini na wewe umefiwa na mwanao katika mazingira ya kutatanisha, hakika mwanao hajafa bali amelala tu, uchumi wako haujafa bali umelala tu, nakwenda kuhamsha uchumi wako, kazi zako. Yamkini na wewe watu wamekucheka sana, wamekudharau leo Bwana anasema hakika karama yako haijafa bali imelala tu.

Biblia inasema: Akamchukuwa baba yake Yule kijana na mama yake, na wale waliopamoja naye, akaingia ndani alipokuwamo Yule kijana, akamshika mkono kijana akamwambia, msichana nakwambia inuka, mara akasimama Yule kijana akaenda, maana alikuwa amepata umri wake miaka kumi na miwili; na mimi leo nakwambia msichana inuka, inuliwa kiuchumi, mahusiano, Bwana ainue kazi zako, biashara zako
SOMA SHUHUDA HIZI ZITAINUA IMANI YAKO

RICHARD MPANGALA ANAMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA AMEWEZA KULIPWA MSHAHARA WAKE WOTE


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Richard Mpangala; kwa kupitia sticker ya Nabii Flora, nilikuwa sijalipwa mshahara kwa muda mrefu, baada tu ya kutumia hii sticker ya Nabii Flora nikalipw amshahara wangu wote, namshukuru sana Mungu.
LEMA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMWONA MCHAWI ANAYEMLOGA MJUKUU WAKE BAADA YA KUOGEA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Lema; namshukuru Mungu kupitia sabuni iliyoombewa na Nabii Flora, siku moja muda wa saa kumi na moja jioni nikaogea hii sabuni iliyoombewa na Nabii Flora, baada ya kumaliza kuoga nikaingia chumbani kwangu nikalala. Dirisha la chumba changu limeelekea nje, ilipofika saa kumi na moja na nusu nikaamka nikachungulia nje, kulikuwa na jirani yangu anaitwa mama Leila vyumba vyetu vinaangaliana milango. Sasa baada ya kuangalia dirishani nikamkuta mama Leila na mjukuu wangu wamekaa wanaangaliana macho, alafu huyo mama Leila akawa amechora kibox chenye pembe nne ile miguu ya mjukuu wangu ameiweka kwenye kibox wanaangaliana macho, alafu akawa anamwambia Yule mjukuu wangu amkazie macho, nikasema Mungu asante umeshanionyesha Yule mchawi anayeloga mjuu wangu. Pia siku ya kwanza mtoto alikuja amepakwa masinzi kwenye kope za macho, nikamwambia Mungu naomba unionyeshe huyu mchawi anayemloga mjukuu wangu, ndio baada tu ya kuogea hiki kipande cha sabuni nikamuona mchawi akiwa na mjukuu wangu. Nikamuuliza unamfanyia nini mjukuu wangu na mbona umeweka miguu ya mjukuu wangu kwenye hichi kibox, akasema mimi simfanyii kitu, basi nikazivunja zile nguvu, na majirani wote wakaja kushuhudia na yeye akaondoka kwa aibu zake.
THERESIA MAIKO ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA TENDA YA KAZI BAADA YA KULETA SAMPO YA BIASHARA YAKO KUOMBEWA KWA NABII FLORA


Bwana Yesu asifiwe, naitwa Theresia Maiko;  nilileta sampo zangu nyingi sana za biashara kwa Nabii Flora, mimi ni mjasiria mali, Nabii aliniombea na baada ya hapo nilipigiwa simu na ubalozi wa Marekani, kwa hiyo kesho naenda kuchukuwa mkataba wa kazi, namshukuru sana Mungu.

ELIZA ANAMSHUKURU MUNGU MTOTO WAKE KAPONA BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA

 Bwana Yesu asifiwe, naitwa Eliza Mkungulwa; nina mtoto wangu alianza kuumwa siku ya Alhamisi, nilimleta jioni kwa Nabii Flora kuombewa. Mtoto alikuwa na hali mbaya sana nikampeleka hospitali lakini hakuwa na ugonjwa wowote, mtoto alikuwa anaumia sana mpaka analia anasema mama nakufa. Nikamleta kwa Nabii Flora akaombewa, mtoto alilala na alipoamka akaanza kuongea na kucheza, namshukuru Mungu sana.
JENIFER MORRIS ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA NA PIA KAPATA KAZI NI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Jenifer Morris; ninamshukuru Mungu kwa kunitendea, nilikuwa nimekata tamaa, nilikuwa ni mtu wa kuumwa sana, kila mwezi nilikuwa nalazwa na ninatumia zaidi ya shilingi laki moja kwaajili ya matibabu. Ilikuwa nikifika kwenye siku zangu ninaumwa sana hata kufanya chochote nilikuwa siwezi, ikafikia mahali mume wangu akasema nirudi kwanza nyumbani nikatibiwe nikipona ndio nirudi. Pia nilikuwa sina kazi nilipokuja kwa Nabii Flora kuombewa Nabii aliniambia nije kwenye ibada ya Jumapili Mungu atanitendea, nilikuja kwenye ibada na baada ya ibada jioni nikapigiwa simu nikaanze kazi, namshukuru sana Mungu kwa kuniponya na nimepata kazi.
LUCY PASCAL ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA MCHUMBA BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Lucy Pascal naishi Salasala; kupitia sticker ya Nabii Flora nimemuona Mungu, namshukuru Mungu nimepata mchumba na ananipenda sana, na ananihudumia mimi pamoja na mtoto wangu ambaye nilizaa na mwanaume mwingine. Na pia kaniambia atanilipia kodi ya nyumba na kila siku ananipa matumizi shilingi elfu thelathini, namshukuru sana Mungu.
CHRIS BALOZI ANAMSHUKURU MUNGU BABA YAKE KAMNUNULIA NYUMBA NI BAADA YA KUTABIRIWA NA NABII FLORA
     Bwana Yesu asifiwe, naitwa Chris Balozi; namshukuru Mungu Nabii alinitabiria mwezi wa kumi na moja nitanunuliwa nyumba na baba, baba yangu alikuwa anipigii simu kabisa na akaniblock kwenye mitandao ya kijamii.

 Lakini namshukuru Mungu baba yangu amerudi na ameninunulia nyumba yenye vyumba sita, sebule mbili na nyumba nyingine ndogo, namshukuru sana Mungu. Na kila siku naingiziwa pesa kwenye account yangu, yaani nikisema tu ninashida pesa zinaingia.
KAROLINE IBRAHIMU ANAMSHUKURU MUNGU AMEPONA SUKARI BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Karoline Ibahimu; nilitumia sticker ya Nabii Flora kwa muda wa wiki mbili, nilikuwa nasumbuliwa sana na sukari, sukari ilishuka ikafikia 20. Lakini namshukuru Mungu baada ya kutumia sticker hii nimepona, na pia matatizo yote kwenye familia yetu yamekwisha.
MAMA VANESSA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA MKOPO BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA PAMOJA NA STICKER
 
Yesu asifiwe, naitwa mama Vanessa; wiki iliyopita nilikuwa ninashida ya pesa kazini kwangu, nikasema office hainiruhusu lakini naomba mkopo. Nilichukuwa sabuni iliyoombewa na Nabii Flora pamoja na sticker nikawa natembea navyo, kweli niliomba mkopo na nikakubaliwa, na wiki hii Mungu kanisaidia nikapata hizo pesa zangu, namshukuru Mungu sana.
BABA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPONA MIGUU BAADA YA KUTUMIA SABUNI ILIYOOMBEWA NA NABII FLORA NA PIA ALIPATA KAZI YA KUSIMAMIA


Bwana Yesu asifiwe; namshukuru Mungu, nilikuwa na hali mbaya sana, kuna dada mmoja alinishuhudia niende kwa Nabii Flora nitaombewa na hali yangu itakuwa nzuri. Kwa kweli nilienda kwa Nabii Flora, siku ya kwanza nikakutana na Mungu wa Nabii Flora, nilikuwa nikitembea napumzika mara mbili au mara tatu, lakini sasa hivi napiga hatua bila wasi wasi. Namshukuru Mungu pia nikapata kazi ya kusimamia kwa siku moja nikalipwa shilingi elfu hamsini.

MARIAMU SALUM ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPONA MALARIA PAMOJA NA PRESSURE BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Mariamu Salum; nilikuwa nikisumbuliewa na malaria kwa muda wa miaka tisa pamoja na pressure ya kushuka, nilikuwa ni mtu wa kuishiwa maji na damu. Lakini mwezi wa kwanza mwaka huu nikaja kwa Nabii Flora nikachukuwa sticker, hii sticker nilikuwa naiweka kwenye mto wakati nalala. Tokea muda huo nilipoanza kuitumia sticker malaria ilikoma, vidonda vilikoma pamoja na pressure ya kushuka, namshukuru sana Mungu.

HAPPY MOSES ANAMSHUKURU MUNGU NDUGU ZAKE WALIOPOTEA KWA MUDA MREFU WAMEREJEA BAADA YA MAOMBI YA NABII FLORA

Bwana Yesu asifiwe, naitwa Happy Moses au mama Witness; Mungu amenitendea sana katika huduma hii ya kuita njoo, nilikuwa na dada zangu wakubwa na wadogo tulikuwa tumepotezana miaka mingi, pamoja na baba yangu mkubwa ambaye aliondoka nyumbani toka mwaka 1982. Sasa tulivyokuwa tunasema njoo mimi nilikuwa nasema tu njoo atakaye kuja ndo huyo huyo maana hata nikitaja jina sijui hata nianze nani. Namshukuru Mungu wale wote niliokuwa nikiwaita njoo walikuja, alianza baba yangu mdogo ambaye alikuwa ni miaka saba alipotea amerudi mwaka huu mwezi wa sita, akafuata mjomba wangu ambaye miaka 15 alikuwa anaishi Malolo amerudi mwaka jana mwezi wa nane, na mwingine ni baba yangu mkubwa kutoka mwaka 1982 yeye anijua na hata mimi simjui, amekuja juzi Dar es salamu kuwatafuta watoto wake, ninamshukuru sana Mungu kwa matendo yake makubwa. Na dada yangu ambaye mwaka 1998 alikuwa anajinyonga mimi nikakata kamba, akasema kwa nini umekata kamba wakati mimi nilitaka nife kwa hiyo kama umekata kamba wewe utashika dhamana ya maisha yangu mimi nilikuwa sitaki kuendelea kuteseka. Nikamwambia dada yangu Mungu anamakusudi na wewe, lakini sasa amejua umuhimu wa kuishi, sasa hivi amekuja ananiambia nakushukuru sana mdogo wangu usingekuwa wewe sasa hivi ningekuwa ni marehemu. Hiyo namtukuza sana Mungu wa madhabahu ya Nabii Flora, ninamuinua sana Mungu amenitendea mambo makubwa na yaajabu.

GRACE ANAMSHUKURU MUNGU KUPONA KUTOKWA NA DAMU BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Grace
; nilikuwa nasumbuliwa sana na kutokwa na damu toka mwezi wa nne, nilipopatwa na matatizo haya niliangaika sana sehemu zote bila mafanikio. Lakini toka nimefika kwa Nabii Flora nikaombewa hivi sasa damu zimekata, namshukuru sana Mungu.

NENO LA MUNGU LINATOKA KATIKA INJILI YA MTAKATIFU MARKO 5:35-42
Biblia inasema: Hata alipokuwa katika kunena, wakaja watu kutoka kwa Yule mkuu wa Sinagogi wakisema, binti yako amekwisha kufa kwa nini kuzidi kumsumbua mwalimu? Lakini Yesu alipolisikia lile neno likinenwa; yamkini hata wewe unaweza kujipenyeza ukafika kwa mtumishi wa Mungu, kuna watu wamekukatisha tamaa, wanakwambia tatizo ulilonalo, tazama kisukari umekwisha kuoza hauweza kupona, mwambie wewe ni mwanadamu tu, inapofikia mwisho wa mwanadamu ndipo mwanzo wa Mungu kutenda. Watu wengi wamekuwa wakikatishwa tamaa, wakivunjwa moyo, usikubali kukatishwa tamaa wewe songa mbele tu.

Biblia inasema: Lakini Yesu aliposikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa Sinagogi, usiogope amini tu, wala hakumruhusu mtu afuatane naye ila Petro na Yohana na Yakobo, wakafika nyumbani kwa Yule mkuu wa Sinagogi. Akaona ghasia na watu wakilia wakifanya maombolezo makubwa, alipokwisha kuingia, akawaambia, mbona mnafanya ghasia na kulia; yamkini hata wewe watu wamekudharau, wanasema tumwone kama atafika popote, hakika nakwambia unakwenda kufika popote, utaona maisha yako yakibadilika, utaona mipango yako inafunguka.

Biblia inasema: Yesu akawaambia kijana hakufa bali amelala tu, wakamcheka sana, naye alipokwisha kuwatoa nje wote; yamkini na wewe umefiwa na mwanao katika mazingira ya kutatanisha, hakika mwanao hajafa bali amelala tu, uchumi wako haujafa bali umelala tu, nakwenda kuhamsha uchumi wako, kazi zako. Yamkini na wewe watu wamekucheka sana, wamekudharau leo Bwana anasema hakika karama yako haijafa bali imelala tu.

Biblia inasema: Akamchukuwa baba yake Yule kijana na mama yake, na wale waliopamoja naye, akaingia ndani alipokuwamo Yule kijana, akamshika mkono kijana akamwambia, msichana nakwambia inuka, mara akasimama Yule kijana akaenda, maana alikuwa amepata umri wake miaka kumi na miwili; na mimi leo nakwambia msichana inuka, inuliwa kiuchumi, mahusiano, Bwana ainue kazi zako, biashara zako.

JINSI YA KUFIKA
Panda magari ya Tegeta ukitokea Makumbusho au Mwenge jijini Dar es Salaam, shuka kituo cha Mbezi Mbuyuni, uliza kanisani kwa Nabii Flora Peter
Tembelea
www.nabiiflora.blogspot.com




Comments