RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ELIZABETH NGAIZA: MUNGU ATAKUBARIKI SANA KAMA UTASAIDIA MASKINI SIKU YA LEO

Mwimbaji wa nyimbo za njili Tanzania Elizabeth Ngaiza ameweza kufanya utafiti na kuona luwa kuna umuhimu mkubwa sana kwa mwanadamu yeyote kumsaidia mwanadamu mwenzake kifedha, kiimani na hata pale anapohitaji msaada wowote. Tanzania na baadhi ya nchi tumegubikwa na umaskini sana na ilifika kipindi mataifa mengine yakawa yanazungumzia mengi juu ya nchi yetu ya Tanzania, wakati ndani ya nchi yetu kuna utajiri mwingi sana ukifananisha na mataifa yaliyoendelea. lakini kinachotushangaza ni kwanini sisi ni maskini?

Elizabeth Ngaiza

Elizabeth Ngaiza katika pitapita zake aliweza kutafuta somo la UMASKINI ambalo hakika ukifuatilia utamuelewa ana maanisha na utajifunza mengi. Naye baada ya kuteseka sana na hali hii ya umaskini aliweza kujikwamua kwa kupata elimu yake kwa shida na sasa Mungu amemuinua ameweza kupata kibali cha kusambaza kazi zake mitaani kwa kutumia gari yake. Fuatilia somo hili la leo kutoka kwa mwanadada huyu wa Yesu

Elizabeth Ngaiza katika gari yake ya kuuzia DVD zake ili kujikwamua na umaskini na kulitangaza Nenola Mungu kwa njia ya uimbaji

Maskini
ni neno ambalo tunalisikia mara kwa mara katika maongezi yetu ya kila siku, tunasikia”Maskini, umaskini, nchi maskini  fukara na nk”.
Futa umasikini
Katika lugha neno maskini lina maana zifuatazo:
  1. Mtu mwenye kipato kidogo ambaye huishi kwa dhiki.
  2. Mtu mwenye ulemavu wa mwili na asiyeweza kujikimu ambaye hutegemea msaada kutoka kwa watu.
  3. Hutumika kama tamko la kumhurumia mtu aliyefikwa na mkasa, baa au tatizo kubwa
Elizabeth Ngaiza akiwa na watoto wenye ulemavu wa nguzi, akiwafariji

Kinyume cha masikini ni Tajiri ambapo neno tajiri lina maana zifuatazo:
  1. Mtu mwenye uwezo,fedha,kipato na mali nyingi.
  2. Mtu aliye ajiri watu ambapo huwalipa mshahara au ujira kwa kazi hiyo.
Wanafalsafa wanatofautiana katika kuelezea maana halisi ya Masikini:
Kuna wanaosema kwamba: masikini ni yule asiyekuwa na uwezo wa kufanya harakati za mfanya kuwa tajiri.
Kundi hili linaamini kwamba: harakati na nguvu za mwanadamu ndio sababu ya kuwa na uwezo au utajiri.
Na wengine wanasema kwamba: masikini ni yule asiyekuwa na uwezo wa kufikiri kujipatia manufaa.
Kundi hili linaamini kwamba utajiri ni kuitumia akili katika kupata manufaa, haijalishi unanguvu au lah.
Kusaidia masikini na wasiojiweza ni kitendo kinachosifiwa katika jamii pia dini na madhehebu mbalimbali,
Dini ya Ukristo na Uyahudi zinasisitiza kutoa sadaka na kusaidia wasiojiweza, hii ni ishara ya kwamba dini hizi zinapinga umasikini.

Elizabeth Ngaiza akiwa na watoto wenye ulemavu wa ngozi.
Dini ya kiislamu pia licha ya kusisitiza kutoa sadaka, inasheria ya kutoa zaka na Khumsi ambazo hutumika kusaidia masikini na wasio jiweza.Wasio kuwa na dini pia hujihisi majukumu ya kusaidia masikini na wasio jiweza.
Hivyo kusaidia wasio jiweza ni hali ya asili kwa mwanadam.Ingawa watu hutofautiana katika kutoa msaada  kuna wanaotoa pesa cha ndogo zaidi zilipo mfukoni mwao, na kuna wanaotoa kiasi cha juu, kuna wanaotoa kwa siri na kuna wanaotoa dhahiri.

Elizabeth Ngaiza
Masikini pia wanatofautiana kuna masikini wenye haja na matatizo lakini hawawezi kuomba kutokana na heshima na shahsia zao, dini ya uislamu inasisitiza watu hawa kutangulizwa mbele katika kuwasaidia,na inasisitiza kutotangaza  misaada wanayopewa.
Pia kuna masikini wanaojitokeza na kuomba msaada, ambapo wapo wenye shida na haja ya kweli na wapo wanaofanya hivyo kama sehemu ya kijipatia fedha.
Ni muhimu kufanya juhudi kuepukana na umasikini, pia ni busara kuwasaidia wasiojiweza msaada wa kutatua kabisa matatizo yao kama itawezekana.
Unadhani nini kinasababisha umasikini, hata ikiafikia nchi zenye hazina kubwa za utajiri kuwa katika orodha ya nchi masikini?

Comments